Pata taarifa kuu

Mapigano nchini Sudan yanaweza kusababisha baa kubwa la njaa: WFP

Nairobi – Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limeonya kuwa vita vinavyoendelea nchini Sudan vinaweza kusababisha kutokea kwa baa kubwa zaidi la njaa duniani iwapo mapigano hayatasitishwa.

WFP pia inataka kuruhusiwa kufika katika maeneo yanayokabiliwa na vita ilikutoa misaada kwa waathiriwa
WFP pia inataka kuruhusiwa kufika katika maeneo yanayokabiliwa na vita ilikutoa misaada kwa waathiriwa REUTERS - EL TAYEB SIDDIG
Matangazo ya kibiashara

Mapigano ya zaidi ya miezi kumi kati ya pande mbili hasimu za kijeshi vimesababisha vifo vya karibia watu 14,000, wengine zaidi ya milioni nane wakiwa wamepoteza makazi yao.

Tayari nusu ya idadi ya watu kwenye taifa hilo wanakabiliwa na tishio la baa la njaa.

Idadi kubwa ya raia wa Sudan wanahamia katika mataifa jirani haswa wakati huu ambapo mapigano yaendelea kuripotiwa.

Wengi wa raia wa Sudan wamekimbilia katika mataifa jirani ya Chad na Sudan Kusini
Wengi wa raia wa Sudan wamekimbilia katika mataifa jirani ya Chad na Sudan Kusini © Karl Schembri/NRC

Wakati akizuru mojawapo ya kambi za wakimbizi wa Sudan katika nchi jirani ya Sudan Kusini, Mkuu wa WFP, Cindy McCain, amsema wathiriwa wa vita hivyo wamesahaulika.

WFP pia inataka kuruhusiwa kufika katika maeneo yanayokabiliwa na vita ilikutoa misaada kwa waathiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.