Pata taarifa kuu

Kongo yazindua uzalishaji wa gesi asilia ya kimiminika

Mamlaka ya Congo Brazzaville na kampuni ya mafuta kutoka Italia ya ENI wamezindua siku ya Jumanne karibu na Pointe-Noire (kusini mwa Kongo) uzalishaji wa gesi ya kimiminika (LNG), ambayo ilikusudiwa kuuzwa nje ya nchi, amebainisha mwandishi wa habari kutoka shirika la habari la AFP.

Bandari inayojiendesha ya Pointe-Noire, nchini Congo-Brazzaville.
Bandari inayojiendesha ya Pointe-Noire, nchini Congo-Brazzaville. © Getty Images/Fabian Plock/EyeEm
Matangazo ya kibiashara

Kwenye eneo la Litchendjili, karibu na mji mkuu wa kiuchumi na wenye mafuta wa Congo Brazzaville, Rais Denis Sassou-Nguesso, akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa kapuni ya Italia ya ENI Claudio Descalzi, amefungua valve, akiashiria kuanza kwa uzalishaji huu.

"Leo tunasherehekea kuanza kwa uzalishaji" na "shehena ya kwanza ya gesi iliyoyeyuka," Bruno Jean-Richard Itoua, Waziri wa mafuta wa Kongo, ameliambia shirika la habari la AFP. Kulingana na waziri huyo, uzalishaji mwaka huu utakuwa tani 600,000 na utaongezeka kutoka mwaka 2025 hadi tani milioni 3 kwa mwaka.

"Tulitaka mradi pamoja na mkandarasi (ENI) ufanyike haraka, kwa sababu kuna soko la gesi linalohitajika sana katika ngazi ya kimataifa," amesisitiza waziri. "Mgogoro kati ya Ukraine na Urusi unaleta mvutano kwenye soko, kwa sababu sehemu ya uzalishaji wa Urusi haipatikani tena," amebainisha. "Kila mzalishaji ana nia ya kusonga haraka ili kuweka gesi yao sokoni," amesema.

Rasmi, mradi huo uligharimu dola bilioni 5 kwa kampuni ya ENI, ambayo tayari ni mzalishaji wa pili wa mafuta nchini Kongo, baada ya kampuni kutoka Ufaransa ya Total. "Teknolojia mpya ilichukua jukumu la msingi katika utekelezaji wa mradi wa LNG wa Kongo katika muda mrefu: mwaka mmoja tu kati ya uamuzi wa mwisho wa uwekezaji na kuanza kwa uzalishaji," Claudio Descalzi amesema.

Kulingana na serikali, uzalishaji huu utaingiza faranga za CFA bilioni 29 (zaidi ya euro milioni 44) katika bajeti ya 2024. Rasilimali ambazo zinatofautiana na maisha ya kila siku ya Wakongo. Kulingana na Benki ya Dunia, karibu nusu ya wakazi wa Kongo wanaishi chini ya mstari wa umaskini na 41% ya vijana wa Kongo hawana ajira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.