Pata taarifa kuu

Wakuu wa nchi za Ecowas wanakutana mjini Abuja

Nairobi – Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanakutana katika kikao cha dharura mjini Abuja, Nigeria, ambapo watajadiliana kuhusu namna ya kutatua mizozo ya kikanda ikiwemo suala la nchi za Burkina Faso, Mali na Niger kutangaza kujitoa kwenye jumuiya hiyo.

Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanakutana katika kikao cha dharura mjini Abuja
Wakuu wa nchi na Serikali kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanakutana katika kikao cha dharura mjini Abuja REUTERS - FRANCIS KOKOROKO
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa mambo mengine yanayotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na hali ya kisiasa katika mataifa ya Niger, Burkina Faso na Mali, nchi zilizochini ya utawala wa kijeshi.

Aidha viongozi hao wanatarajiwa kuamua ikiwa waiondolee vikwazo nchi ya Niger, vikwazo ambavyo iliwekewa tangu wanajeshi waipindue serikali ya rais Mohammed Bazoum.

Tayari mawakili wa rais Bazoum wametuma ombi kwa Ecowas wakitaka ishinikize kuachiwa kwa mteja wao.

Kinachoendelea nchini Senegali pia huenda kikawa miongoni mwa agenda za mkutano wa Abuja, maazimio ya nchi wanachama yakitarajiwa kutoa mwelekeo wa muungano huo katika siku zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.