Pata taarifa kuu

Rais Tshisekedi kufuatlia kwa karibu kesi ya mwanahabari Stanis Bujakera

Mwandishi wa habari nchini DRC Stanis Bujakera, aliyekamatwa Septemba 8, 2023, "labda [...] anadidimizwa" gerezani kwa sababu ya "kutowajibika kwa vyombo vya sheria nchini DRC, Rais Antoine-Felix Tshisekedi alibaini Februari 22, 2024, ambaye alisema ameamua "kufuatilia kwa karibu kesi hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi akiwasili kabla ya hafla ya ufunguzi wa kikao cha 37 cha kawaida cha mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Februari 17, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Félix Tshisekedi akiwasili kabla ya hafla ya ufunguzi wa kikao cha 37 cha kawaida cha mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) katika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa, Februari 17, 2024. AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Mwandishi wa habari wa Gazeti la Jeune Afrique, Stanis Bujakera anasikilizwa mahakamani tangu Oktoba 13, 2023 kwa makala ambayo haijatiwa saini katika gazeti hili inayohusisha ujasusi wa kijeshi na kifo cha mwanasiasa wa upinzani, Chérubin Okende.

Mwandishi huyo wa Kongo, anayezuiliwa kwa zaidi ya siku 160 na anasikilizwa na mahakama kwa makala iliyochapishwa na ambayo haijatiwa saini katika Gazeti la Jeune Afrique inayohusisha ujasusi wa kijeshi katika mauaji ya waziri wa zamani Chérubin Okende, ni mwathiriwa wa "vyombo vya sheria visivyo wajibika".

Haya ni mahitimisho ya rais wa nchi hiyo, Félix Tshisekedi, ambaye alikuwa mbele ya waandishi wa habari, akiwemo mwanahabari wetu Pascal Mulegwa, Februari 22, 2024 mjini Kinshasa.

Mkuu wa nchi aliahidi "kufuatilia kwa karibu" kesi hiyo hadi mwisho, huku akitarajiwa kusikilizwa tena leo Ijumaa, Februari 23 katika gereza kuu la Makala katika kesi hii.

"Kwa sababu ya kukawia kwao, labda kijana huyu anaishia jela."

"Vyombo vyetu vya sheria vinaumwa, hata katika kushughulikia kesi," alitangaza Félix Tshisekedi. Na nadhani yeye ni mwathirika wa hilo. Niliamua kweli kufuatilia kesi hiyo. Sipendi kufanya hivyo, mniamini. Naapa: Sijawahi kutoa wito kwa majaji, nina imani nao. Nasisitiza tu wasome sheria na kutekeleza kile ambacho inasema, ili wenzetu wananchi wanufaike nayo.”

Rais, ambaye aliapishwa kwa muhula wa pili Januari 20, anaendelea:

"Ninahitaji haki ambayo ni sahihi, ambayo ni madhubuti, kwa sababu ndivyo ilivyo. Ni kwa haki hii tutajenga utawala wa sheria tunaoutaka, hivyo nataka haki hii. Kwa sababu ya kukawia kwao, pengine kijana huyu anaishia gerezani. Ninawaambia kwa dhati: Nimeamua kufuatilia kesi hiyo angalau mara moja. Mengi zaidi nitajua kesho kwa sababu nitapata majibu kuanzia kesho. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.