Pata taarifa kuu

Somalia yaidhinisha makubaliano ya ulinzi na Uturuki

Serikali ya Somalia na bunge wameidhinisha makubaliano ya ulinzi na Uturuki siku ya Jumatano, dhidi ya hali ya mvutano wa kikanda kati ya Mogadishu na jirani yake Ethiopia ambayo ilitia saini makubaliano na eneo linalojitenga la Somalia la Somaliland.

Mwanajeshi wa jeshi la Somalia akipigwaa picha huko Baidoa.
Mwanajeshi wa jeshi la Somalia akipigwaa picha huko Baidoa. AFP - GUY PETERSON
Matangazo ya kibiashara

"Chini ya makubaliano ya ulinzi wa miaka 10, Uturuki, mwanachama wa NATO na mshirika wa karibu wa Somalia, itasaidia kutetea ukanda mrefu wa pwani ya Somalia na kuanzisha upya vikosi vya wanamaji vya nchi hiyo isiyo na utulivu. ya Pembe ya Afrika", ameeleza Rais Hassan Cheikh Mohamoud kufuatia kikao cha pamoja na Bunge.

"Makubaliano yaliyowasilishwa Bungeni leo yanahusu tu ushirikiano kati ya Somalia na Uturuki katika ulinzi wa bahari na masuala ya kiuchumi, hayakusudiwi kwa vyovyote kujenga chuki au ugomvi na nchi au serikali nyingine yoyote," amesema.

Mvutano umekuwa mkubwa kati ya majirani katika Pembe ya Afrika tangu maelewano kati ya Ethiopia na Somaliland, yaliyotokea kwa kutiwa saini Januari 1 ya "mkataba wa maelewano" unaotoa nafasi kwa Ethiopia kukodisha kwa miaka 50 kwa pwani ya kilomita 20 ya Somaliland katika Ghuba ya Aden. Mogadishu ilishutumu makubaliano "haramu".

Mamlaka ya Somaliland ilithibitisha kwamba badala ya upatikanaji huu wa bahari, Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua rasmi, jambo ambalo halijafanyika tangu eneo hili dogo lenye wakazi milioni 4.5 kutangaza uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991.

"Makubaliano ya kihistoria"

"Somalia imeeleza kwa uwazi msimamo wake: mamlaka na ukamilifu wa eneo la Somalia kamwe hauwezi kujadiliwa, na hii imesababisha leo kufikia makubaliano haya ya kihistoria," naibu waziri ameliami shirika la habari la AFP. "Kwa makubaliano haya, Uturuki italinda pwani ya Somalia dhidi ya maharamia, magaidi (...) kutoka kwa wale wote wanaokiuka mipaka yetu ya baharini kama Ethiopia," ameongeza.

Ankara inadumisha uhusiano wa karibu na Somalia na ni mshirika wake mkuu wa kiuchumi, haswa katika sekta ya ujenzi, elimu na afya na vile vile katika ushirikiano wa kijeshi. Somalia pia knapatikana kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Uturuki na kituo cha mafunzo ya nje ya nchi, kulingana na vyombo vya habari vya Uturuki.

Kufuatia kusainiwa kwa makubaliano kati ya Somaliland na Ethiopia, nchi nyingi na mashirika ya kimataifa (Marekani, China, Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Kiarabu) wametoa wito wa kuheshimiwa kwa uhuru wa Somalia. Nchi ya pili kwa idadi kubwa ya watu barani Afrika (wakazi milioni 120), Ethiopia inatafuta ufikiaji wa Bahari Nyekundu, ambayo ilipoteza hatua kwa hatua baada ya uhuru wa Eritrea mnamo 1993 - ambayo iliichukua miaka ya 1950.

Eneo ambalo ni tulivu ikilinganishwa na nchi nyingine ya Somalia, ambayo imekuwa katika machafuko kwa miongo mitatu, jamhuri inayojiita ya Somaliland ina taasisi zake, inachapisha sarafu yake na kutoa hati zake za kusafiria, lakini ukosefu wa kutambuliwa kimataifa unaiweka katika hali ya wasiwasi ya kutengwa kimataifa.

Eneo hili linaendelea kuwa maskini licha ya eneo lake la kimkakati kwenye ufuo wa kusini wa Ghuba ya Aden, kwenye mojawapo ya njia zenye shughuli nyingi zaidi za biashara duniani, kwenye lango la Mlangowa Bahari wa Bab-el-Mandeb unaoelekea Bahari Nyekundu na mfereji wa Suez.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.