Pata taarifa kuu

Jeshi la maji la Morocco limethibitisha kuwaokoa wahamiaji 141 wa Afrika

Nairobi – Maofisa wa jeshi la maji nchini Morocco wamewaokoa wahamiaji 141 wa Afrika kutoka kwenye boti walimokuwa wakisafiria iliokumbwa na changamoto wakati wakielekea katika visiwa Canary nchini Uhispania wakitokea nchini Mauritania.

Bateau en provenance du Maroc sur une plage de Gran Canarias, en octobre 2020 (Image d'illustration).
Bateau en provenance du Maroc sur une plage de Gran Canarias, en octobre 2020 (Image d'illustration). © AP - Javier Bauluz
Matangazo ya kibiashara

Shughuli ya kuwaokoa wahamiaji hao imefanyika hapo jana Jumapili kilomita 274 Kusini Magharibi mwa mji wa Dakhla-Magharibi mwa jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa uongozi wa jeshi la maji la Morocco, wahamiaji hao waliondoka pwani ya Mauritania tarehe 10 ya mwezi Februari.

Mwaka uliopita, visiwa vya Canary viliripotiwa kuwapokea karibia wahamiaji elfu 32, idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa tangu mwaka wa 2006.

Mwezi Januari, mamlaka nchini Uhispania iliripoti kuendelea kuandikisha idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili katika visiwa hivyo, sehemu kubwa ya boti za wahamiaji zikitokea nchini Mauritania.

Idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakiripotiwa kuzama wakijaribu kuvuka kwenda bara Ulaya kutoka bara Afrika wakitumia njia hatari zikiwemo boti za mbao.

Wengi wa wahamiaji wanasema wanataka kwenda barani Ulaya kutafuta maisha bora kutokana na ugumu wa maisha na nafasi chache za ajira katika baadhi ya nchi za Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.