Pata taarifa kuu

Wakuu wa nchi za Afrika kuhudhuria kikao cha kawaida cha 37 nchini Ethiopia

Nairobi – Wakuu wa mataifa ya Afrika wameanza kuwasili jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, kuhudhuria kikao cha kawaida cha 37 cha wakuu wa nchi, kesho na Jumapili.

Wakuu wa nchi za Afrika kufanya kikao jijini Addis Ababa
Wakuu wa nchi za Afrika kufanya kikao jijini Addis Ababa © MFA ETHIOPIA
Matangazo ya kibiashara

Kwanza kikao hiki kinafanyika baada ya wanachama wake wawili Gabon na Niger kushuhudia mapinduzi ya kijeshi kwa kipindi cham waka mmoja uliopita, lakini pia mzozo wa kisiasa nchini Senegal, baada ya uchaguzi uliokuwa ufanyike mwezi huu kuahirishwa.

Wakuu wa nchi za Gabon na Niger, hawatakuwepo jijini Addis Ababa baada ya nchi zao kusimamishwa uanachama kama ilivyo kwa Mali, Guinea, Sudan na Burkina Faso.

Namna ya kutatua mizozo ya kisiasa na usalama katika nchi hizo bila kusahau kinachoendelea Mashariki mwa DRC na Somalia, ni swali kubwa linalotarajiwa kutawala kikao hicho, lakini wachambuzi wa mambo wanahoji uwezo wa wakuu hao kuja na maamuzi yatakayosaidia kuleta suluhu ya kudumu.

Kikao hiki kinafanyika pia kwenye mwaka ambao kuna uchaguzi Mkuu 19 katika nchi mbalimbali za Afrika mwaka huu wa 2024, suala ambalo linaelezwa kuzua changamoto kuhusu uthabiti wa kisiasa wa nchi hizo.

Suala lingine tata ni kuhusu namna Umoja wa Afrika unavyoweza kuanza kujitegemea kifedha kutoka nchi wanachama badala ya kuwategemea wahisani wa Kimataifa.

Mwenyekiti wa sasa wa Umoja huo rais wa Comoro Azali Assoumani anatarajiwa kukabidhi kijiti kwa rais wa Mauritania Mohamed Ould Ghazouani kushika nafasi hiyo kwa mwaka mmoja ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.