Pata taarifa kuu

Senegal: Kati ya ofisi ya rais na Ousmane Sonko, mazungumzo sasa yanawezekana

Je, Senegal inaweza kuelekea katika utulivu? Siku kumi baada ya tangazo la Rais Macky Sall kuahirisha uchaguzi wa urais, upinzani na mashirika ya kiraia wameenelea kuonyesha hasira zao, hata kama utulivu unatawala katika mji mkuu. Nyuma ya pazia, ofisi ya rais ilianza mazungumzo na kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko kujaribu kupunguza mvutano.

Rais wa Senegal Macky Sall na kiongozi wa upinzani wa serikali Ousmane Sonko.
Rais wa Senegal Macky Sall na kiongozi wa upinzani wa serikali Ousmane Sonko. © Montage RFI - AP/Johanna Geron - AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Wasuluhishi walianza kuziba pengo kati ya Macky Sall na Ousmane Sonko ambaye yuko gerezani tangu mwezi Julai. Mwanaharakati wa haki za binadamu Alioune Tine na mfanyabiashara Pierre Goudiaby Atepa ndio  wasuluhishi. Pierre Goudiaby Atepa anaeleza kwamba "aliteuliwa kuwa mwezeshaji na rais kuona jinsi ya kumshawishi kila mtu kwa ajili ya mazungumzo kwa lengo la kutuliza uhasama". Suala la kuachiliwa kwa Ousmane Sonko liko mezani na mazungumzo tayari yanaendelea. Kulingana na Pierre Goudiaby Atepa, Rais Macky Sall tayari ametoa maagizo yake ya kuwaachilia katika siku zijazo karibu watu elfu moja wanaozuiliwa jela baada ya kukamatwa mwezi Machi na Juni mwaka uliyopita.

Kwa upande wa chama cha kiongozi wa upinzani, PASTEF kilichofutwa, wanasema hawaombi chochote: wala mazungumzo wala msamaha. "Tunataka uchaguzi haraka iwezekanavyo," anasema kada wa chama ch zamani cha PASTEF.

Ishara nyingine ya utulivu: urejeshaji wa data za simu ambazo zilikatwa siku ya Jumanne Februari 13, na ishara ya televisheni ya Walf TV siku ya Jumatatu ambayo leseni yake ilirejeshwa mamlakani kando ya maandamano siku ya Ijumaa.

Lakini kwa sasa, ishara hizi hazishawishi kila mtu. Sehemu kubwa ya upinzani bado inataka uchaguzi ufanyike Februari 25 na kuondoka kwa Macky Sall Aprili 2, tarehe ambayo alipaswa kukabidhi madaraka kwa mrithi wake.

Baraza la Katiba linatarajia kutoa uamuzi kuhusu rufaa zilizowasilishwa na wagombea kupinga sheria inayoweka tarehe mpya ya uchaguzi mnamo Desemba 15. Macky Sall hadi sasa hajaonyesha dalili yoyote ya kurejelea uamuzi wake. Na muungano mpya wa mashirika ya kiraia wa Aar Sunu Elections bado unapanga maandamano siku ya Jumamosi Februari 17 kote nchini kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.