Pata taarifa kuu

Miili ya wanajeshi wa UAE waliouawa Somali imewasili Abu Dhabi

Nairobi – Miili ya wanajeshi watatu kutoka milki ya falme za kiarabu waliouawa katika shambulio la kigaidi nchini Somalia, imewasili huko Abu Dhabi.

Serikali ya Somalia mwezi Agosti mwaka wa 2022 ilitangaza vita vikali dhidi ya kundi la Al-Shabab
Serikali ya Somalia mwezi Agosti mwaka wa 2022 ilitangaza vita vikali dhidi ya kundi la Al-Shabab AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Taarifa imeeleza kuwa mwanajeshi wa nne aliyejeruhiwa wakati wa shambulio hilo la siku ya Jumamosi, alifariki baada ya kuwasili UAE.

Mamlaka imeeleza kuwa maofisa hao wa jeshi walikuwa nchini Somalia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa ndani.

Afisa mwengine wa jeshi la Bahrain aliripotiwa kuuawa katika shambulio hilo ambalo wapiganaji wa al-Shabab walikiri kuhusika.

Jeshi la Bahrain katika taarifa yake limekashifu mauaji ya afisa wake likisema ni kitendo cha kichokozi.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya ndani, shambulio hilo lilitekelezwa na afisa wa jeshi ambaye alikuwa akiishi kwenye kambi ya jeshi baada ya kuondoka kwenye kundi la al-Shabab.

Shambulio lilitokea katika kambi ya jeshi ya General Gordon jijini Mogadishu.

Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud amelaani shambulio hilo akiwataka maofisa wa serikali yake kuanzisha uchunguzi wa kina katika tukio hilo.

Wapiganaji wa Al-Shabab wameendelea kutekeleza mashambulio mabaya nchini Somali licha ya serikali kutangaza vita vikali dhidi ya kundi hilo mwezi Agosti mwaka wa 2022.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.