Pata taarifa kuu

Ethiopia: Marekani inasema imeguswa na ripoti za mauaji ya kikabila

Nairobi – Marekani imeeleza kuguswa na kile inachosema ni kuwepo kwa ripoti za mauaji ya yanayowalenga baadhi ya raia katika mji wa kaskazini mwa nchi ya Ethiopia.


Wasiwasi iliibuka zaidi katika mji wa Amhara mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza kuvivunja vikosi vya eneo hilo
Wasiwasi iliibuka zaidi katika mji wa Amhara mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed kutangaza kuvivunja vikosi vya eneo hilo © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kutokana na ripoti hiyo, Washington imetoa wito kwa mamlaka nchini Ethiopia kuruhusu vitengo vinavyohusika na masuala ya haki binadamu kuwasili kwenye mji huo kuchunguza madai hayo.

Taarifa ya kuwepô kwa mauaji ya aina hiyo katika eneo la Merawi kwenye mji wa Amhara, imekuja baada ya kuripotiwa kwa makabiliano ya miezi kadhaa mwaka uliopita kati ya jeshi la serikali na wapiganaji wa kabila la Amhara maarufu kama Fano.

Mwezi Agosti mwaka wa 2023, serikali ya shirikisho ilitangaza hali ya dharura katika mji wa Amhara kutokana na machafuko yaliokuwa yakiendelea, muda ambao uliongezwa kwa miezi minne na wabunge wiki iliopita.

Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti kwamba raia waliauwa na wanajeshi wa serikali ambao walikuwa wakienda nyumba baada ya nyumba kuwatafuta watu wanaodaiwa kushirikiana na wapiganaji wa Fano.

Licha ya taarifa hiyo ya vyombo habari kwenye eneo hilo, imekuwa vigumu kuthibitisha madai hayo kufuatia hatua ya serikali kudhibiti shughuli za wanahabari kwenye eneo husika.

Wasiwasi iliibuka zaidi katika mji wa Amhara mwezi Aprili mwaka uliopita baada ya waziri mkuu Abiy Ahmed na serikali yake kutangaza kuvivunja vikosi vya eneo hilo, hali ambao ilizua maandamano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.