Pata taarifa kuu

Senegal: Wabunge watatu wa upinzani wanazuiliwa na polisi

Nairobi – Wanasiasa watatu wa upinzani nchini Senegal wanazuiliwa na polisi wakihusishwa na mvutano uliotokea bungeni kufuatia hatua ya kuhairishwa kwa tarehe ya uchaguzi wa urais kwa miezi kumi.

Tume ya ECOWAS tayari imetoa wito kwa mamlaka kwenye taifa hilo kutangaza kalenda mpya ya uchaguzi
Tume ya ECOWAS tayari imetoa wito kwa mamlaka kwenye taifa hilo kutangaza kalenda mpya ya uchaguzi AP - Stefan Kleinowitz
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa msemaji wa chama kilichofutwa cha Pastef, El Malick Ndiaye, wabunge watatu wanaoshikiliwa ni wa kutoka kwa muungano wa vyama vya upinzani wa Yewwi Askan Wi na walikamatwa siku ya Jumanne.

Wabunge nchini Senegal siku ya Jumatatu, walipiga kura kuunga mkono pendekezo la rais Macky Sall na kusongezwa mbele kwa kalenda ya uchaguzi, hatua ambayo sasa inampa kiongozi huyo nafasi ya kusalia madarakani hadi kutakapofanyika uchaguzi mwengine.

Rais Macky Sall amesisitiza kuwa hana nia ya kuwania tena katika uchaguzi ujao
Rais Macky Sall amesisitiza kuwa hana nia ya kuwania tena katika uchaguzi ujao © AP/Christophe Ena

Wakati wa mjadala huo kwenye bunge, sehemu kubwa ya wabunge wa upinzani waliondolewa bungeni baada ya kutokea kwa makabiliano.

Hatua ya kuhairishwa kwa uchaguzi huo imezua maadamano jijini Dakar, wito ukiendelea kutolewa kutoka kwa jamii ya kimataifa kwa mamlaka nchini Senegal kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kama ilivyopangwa.

Hatua ya kusongeza mbele tarehe ya uchaguzi ilizua maandamano jijini Dakar
Hatua ya kusongeza mbele tarehe ya uchaguzi ilizua maandamano jijini Dakar AFP - JOHN WESSELS

Tume ya ECOWAS tayari imetoa wito kwa mamlaka kwenye taifa hilo kutangaza kalenda mpya ya uchaguzi kwa mujibu kwa katiba ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.