Pata taarifa kuu

Senegal : Wabunge waidhinisha kuahirishwa kwa uchaguzi mkuu

Nairobi – Wabunge nchini Senegal wamepitisha muswada wa kuahirisha uchaguzi wa rais hadi Desemba 15, mwaka huu wa 2024 na kuongeza mamlaka zaidi kwa rais anayemaliza muda wake Macky Sall, hatua iliyozua vurugu ndani ya bunge hapo jana jijii Dakar.

Kulikuwa na ulinzi mkali jijini Dakar wakati wa kikao cha kujadili muswada huo kwenye bunge
Kulikuwa na ulinzi mkali jijini Dakar wakati wa kikao cha kujadili muswada huo kwenye bunge AP - Sylvain Cherkaoui
Matangazo ya kibiashara

Muswada huo wa kuahirishwa kwa uchaguzi Mkuu nchini Senegal hadi Desemba 15 mwaka huu wa 2024 ulifikiwa baada ya wabunge walioonekana kuunga mkono utawala wa rais anayemaliza muda wake Macky Sall pamoja na wapinzani kukabiliana.

Maafisa wa polisi walilazimika kuingilia mara moja mvutano huo na kuwatoa nje wabunge wa upinzani, ambao walionekana kutounga mkono tarehe hiyo, na pia kuongezewa mamlaka zaidi kwa rais huyo.

Hatua ya rais Sall kuhairisha tarehe ya uchaguzi mkuu imeibua maandamano
Hatua ya rais Sall kuhairisha tarehe ya uchaguzi mkuu imeibua maandamano © AFP - SEYLLOU

Ayib Daffé ni mbunge wa zamani wa chama cha upinzani cha Pastef kinachoongozwa na kinara wa Upinzani Ousmane Sonko.

"Mnawezaji kufanyika katiba yetu marekebisho na kuvunja utaratibu wa kanunu za ndani." alisema

Ayib Daffé ni mbunge wa zamani wa chama cha upinzani cha Pastef.

00:37

Ayib Daffé - mbunge wa zamani wa chama cha upinzani cha Pastef

Senegal imekumbwa na mzozo wa kisiasa tangu Rais Sall kutangaza kuchelewesha uchaguzi huo wa rais siku ya Jumamosi, masaa machache kabla ya kampeni kuanza rasmi.

Viongozi wa upinzani wameilaani hatua hiyo na kusema ni “mapinduzi ya kikatiba”, wakisema ni ukandamizaji wa demokrasia.

Licha ya hatua hiyo rais Sall amesisitiza kuwa hana nia ya kuwania tena kwenye uchaguzi mkuu ujao
Licha ya hatua hiyo rais Sall amesisitiza kuwa hana nia ya kuwania tena kwenye uchaguzi mkuu ujao AFP - SEYLLOU

Wabunge 105 walipigia kura kuunga mkono pendekezo hilo.

Hapo awali ilipendekezwa kuahirishwa kwa miezi sita, lakini marekebisho ya dakika za mwisho yalirefusha hadi miezi 10, au 15 Desemba.

Sall alikariri kwamba hakuwa na mpango wa kuwania wadhifa huo tena. Lakini wakosoaji wake wanamshutumu kwa kujaribu kung'ang'ania mamlaka pamoja na kutekeleza mageuzi yanayolenga kumnufaisha mrithi wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.