Pata taarifa kuu
KENYA - TAMASHA

Kenya : Tamasha la wanahabari Africa

NAIROBI –  Taasisi ya Baraza Media Lab nchini Kenya, inajiandaa kuwa mwenyeji wa awamu ya pili ya tamasha la wanahabari barani Africa, tamasha litakalofanyika mwezi huu tarehe 21 na 22, hafla itakayofanyika katika kituo cha makumbusho ya kitaifa jijini Nairobi.

Wasimamizi wanaofanikisha Tamasha la wanahabari barani Africa.
Wasimamizi wanaofanikisha Tamasha la wanahabari barani Africa. © Baraza media lab
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wanahabari 300 wanatarajiwa kongamana jijini Nairobi kuhudhuri tamasha la mwaka huu kutoka mataifa 18 ya Africa, lengo likiwa kuwaleta pamoja wadau mbali mbali kujadili hali ya baadaye ya wanahabari barani , ambapo changamoto na mafanikio ya wanahabari wa Africa yatajadiliwa kwenye tamasha hilo la siku mbili.

Wadau wa Bazara Media Lab, wakati wa uzinduzi wa ripoti 06 02 2024
Wadau wa Bazara Media Lab, wakati wa uzinduzi wa ripoti 06 02 2024 © Baraza media lab

Kwa mjibu wa Christine Mungai, mmoja wa waandalizi wakuu wa hafla hii, ni kwamba wanalenga kuwakutanisha wanahabari kutoka kote barani Africa ambapo watakutana na kujadili maswala mbalimbali ambayo huwaandama  katika shughuli zao za kila siku.

00:49

CHRISTINE MUNGAI

Aidha imebainika kwamba huenda tamasha zitakazofuata zikandaliwa katika mataifa mengine ya Africa, baada ya nchi ya Rwanda kuonesha nia ya kutaka kuwa mwenyeji wa tamasha hilo.

 

Mbali na wanahabari patawepo pia watatumbuizaji kutoka kwa wacheshi wanamuziki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.