Pata taarifa kuu

Bemba: 'Kila kitu kinafanywa ili kuhakikisha kwamba Goma haianguki mikononi mwa waasi'

Rais Félix-Antoine Tshisekedi alikutana siku ya Jumatatu, Februari 5 jioni na Baraza Kuu la Ulinzi ili kujadili masuala ya usalama nchini kote, hasa katika mkoa wa Kivu Kaskazini, kwa mujibu wa Radio Okapi ikunukuu Jean-Pierre Bemba, Naibu Waziri Mkuu akiwa pia Waziri wa Ulinzi wa DRC.

Jean-Pierre Bemba, Naibu Waziri Mkuu akiwa pia Waziri wa Ulinzi wa DRC wakati wa mkutano huko Kinshasa mnamo Aprili 29, 2023.
Jean-Pierre Bemba, Naibu Waziri Mkuu akiwa pia Waziri wa Ulinzi wa DRC wakati wa mkutano huko Kinshasa mnamo Aprili 29, 2023. AFP - ARSENE MPIANA
Matangazo ya kibiashara

 

“Kila kitu kinafanywa kuhakikisha kuwa jiji la Goma halianguki mikononi mwa waasi. Jeshi pia linafanya kila linalowezekana kurejesha maeneo yote yanayokaliwa na wanajeshi wa Rwanda,” alisema Jean-Pierre Bemba baada ya mkutano huo.

Baraza Kuu la Ulinzi limetoa wito kwa watu kutulia kutokana na tetesi mbalimbali kuhusiana na uvamizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

"Lazima tuwe waangalifu na mitandao ya kijamii ambayo inaleta hofu fulani, udhaifu katika akili za watu. Tuwe waangalifu, hii sio ukweli. Adui anatumia mbinu hiyo kwa kupitia mitandao mbalimbali. FARDC inafanya kazi ya ajabu. Adui anapata hasara kubwa,” aliongeza Jean-Pierre Bemba.

Baraza Kuu la Ulinzi lilimtaka Félix Tshisekedi "kufuta sheria ya kusitishwa kwa adhabu ya kifo, kuhusiana na maswali ya usaliti ndani ya vikosi vya Ulinzi na Usalama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.