Pata taarifa kuu

Senegal: AU yatoa wito wa kufanyika mazungumzo katatua mzozo wa kisiasa

Nairobi – Mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ametoa wito wa kusuluhishwa kwa mizozo ya kisiasa nchini Senegal kupitia njia ya mazungumzo na mashauriano.

Kulizuka maandamano jijini Dakar baada ya agizo la rais Sall kusongesha mbele tarehe ya uchaguzi mkuu wa urais.
Kulizuka maandamano jijini Dakar baada ya agizo la rais Sall kusongesha mbele tarehe ya uchaguzi mkuu wa urais. © AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Wito wa AU umekuja baada ya kushuhudiwa makabiliano kufuatia hatua ya kuhairishwa kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwezi huu.

Faki aidha ametoa wito kwa mamlaka kuandaa uchaguzi huo haraka kama ilivyopangwa na kwa njia ya uwazi na haki

Rais wa Senegal Macky Sall alitangaza kuwa uchaguzi wa tarehe 25 ya mwezi Februari umehairishwa.

Hatua ya rais Sall kuhairisha tarehe ya uchaguzi mkuu imeibua maandamano
Hatua ya rais Sall kuhairisha tarehe ya uchaguzi mkuu imeibua maandamano © AFP - SEYLLOU

Wito wa AU unakuja wakati huu pia wabunge nchini humo wakitarajiwa pia kukutana kujadili hatua hiyo ya Sall ambayo imeibua mzozo kwenye taifa hilo.

Wabunge hao wanakutana siku moja baada ya kutokea kwa maandamano jijini Dakar, tukio ambalo lilipelekea kukamatwa kwa mwanasiasa wa upinzani.

Rais Macky Sall alieleza kuwa alichukua hatua hiyo kwa sababu ya mzozo uliopo kati ya mahakama ya katiba na baadhi ya wagombea
Rais Macky Sall alieleza kuwa alichukua hatua hiyo kwa sababu ya mzozo uliopo kati ya mahakama ya katiba na baadhi ya wagombea © Capture d'écran Facebook / Macky Sall

Rais Sall katika taarifa yake ya Jumamosi ya wiki iliopita, alieleza kuwa amechukua hatua ya kusongesha mbele tarehe ya uchaguzi mkuu kwa sababu ya mzozo kati ya bunge la kitaifa na mahakama ya kikatiba kuhusiana na suala la baadhi ya wagombea kuzuiliwa kuwania.

Mahakama ya katiba ilimzuia Karim Wade, mwanawe rais wa zamani Abdoulaye Wade kutowania katika uchaguzi mkuu wa urais.

Wade alizuiliwa kwa madai ya kuwa na uraia wa nchi ya Ufaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.