Pata taarifa kuu

Niger: Zaidi ya watu 20 wameauwa katika shambulio: Ripoti

Nairobi – Karibia raia 22 wameuawa na watu wanaodhaniwa kuwa wapiganaji wa kijihadi kwenye kijiji kimoja nchini Niger karibu na mpaka wa taifa hilo na Mali.

Niger imekuwa ikakabiliwa na changamoto wa wanajihadi tangu mwaka wa 2015
Niger imekuwa ikakabiliwa na changamoto wa wanajihadi tangu mwaka wa 2015 AFP - ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa afisa kwenye eneo hilo, watu wenye silaha waliokuwa wakitumia usafiri wa pikipiki, waliwashambulia raia kwa risasi kwenye kijiji cha Motagatta katika sekta ya Tillaberi.

Hadi tukichapisha taarifa hii, haikuwa imebainika ni akina nani walitekeleza shambulio hilo, utawala wa kijeshi nchini Niger nao pia haukuwa umezungumzia suala hilo.

Mashambulio kama haya ni kawaida nchini Niger, nchi ambayo imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya makundi ya watu wenye silaha tangu mwaka wa 2015.

Utawala wa kijeshi nchini Niger ulisema ulitekeleza mapinduzi kwa sababu ya kuendelea kudorora kwa hali ya usalama
Utawala wa kijeshi nchini Niger ulisema ulitekeleza mapinduzi kwa sababu ya kuendelea kudorora kwa hali ya usalama REUTERS - STRINGER

Karibia wanajeshi 40 waliuawa mwaka jana katika mashambulio tofauti katika eneo la mpaka wa nchi hiyo na Burkina Faso.

Uongozi wa kijeshi ulitekeleza mapinduzi mwaka uliopita kwa madai kuwa hali ya usalama kwenye taifa hilo la Sahel ilikuwa imedorora.

Mwezi Desemba, Kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdourahamane Tiani, alieleza kuwa hali ya usalama ilikuwa imeanza kuwa sawa baada ya maofisa wake kuanza harakati za kuwakabili watu wenye silaha.

Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger
Jenerali Abdourahamane Tiani- Kiongozi wa kijeshi nchini Niger AP

Wanajeshi wa Ufaransa wameondoka jijini Niamey baada ya kutakiwa kufanya hivyo na utawala wa kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.