Pata taarifa kuu

Senegal: Ousmane Sonko amchagua Faye kupeperusha bendera ya PASTEF katika uchaguzi wa urais

Vyombo vya habari vya Senegal vimerusha video isiyojulikana tarehe iliyorekodiwa inayohusishwa na kiongozi wa upinzani anayefungwa Ousmane Sonko ambapo anamtaja naibu wake Bassirou Diomaye Faye kama atakayechukuwa nafasi yake katika uchaguzi wa urais wa Februari 25. Bw. Sonko pia anatoa wito wa kuachiliwa kwa Bw. Faye, ambaye pia anazuiliwa.

[Picha ya kumbukumbu] Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, mjini Dakar mnamo Machi 8, 2021.
[Picha ya kumbukumbu] Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, mjini Dakar mnamo Machi 8, 2021. AFP - SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

 

Video iliyorushwa kwenye ukurasa wa Facebook wa Bw. Sonko na kwenye kituo cha televisheni cha Jotna, che ukaribu na kiongozi huyo wa upinzani, haibainishi tarehe iyorekodiwa. Wiki iliyopita walitangaza kwa njia kama hiyo video iliyorekodiwa kulingana na Bw. Sonko  kwa kutarajia kutoweza kwake kushiriki katika uchaguzi wa urais. Bw. Sonko, aliyetangazwa kuwa mmoja wa watu wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kushinda katika uchaguzi huo, alifungwa Julai 2023 kwa kuitisha uasi, njama ya uhalifu inayohusishwa na biashara ya kigaidi na kuhatarisha usalama wa taifa.

Tangu mwaka 2021, kuhusika kwake katika kesi za kisheria ambazo anaona kama njama iliyotengenezwa ya kutaka kumtega katika uchaguzi huo, na mvutano wake na mamlaka kumesababisha machafuko mabaya. Bw. Sonko ameondolewa tu kwenye uchaguzi wa urais na Baraza la Kikatiba.

Ugombea wa Bw. Faye ulikuwa tayari mpango B wa Bw. Sonko na chama chake kilichofutwa, PASTEF, ingawa Bw. Faye pia anafungwa tangu mwezi Aprili 2023. Baraza la Katiba, kwa upande mwingine, limethibitisha kugombea kwake, kwa sababu, tofauti na Bw. Sonko, hajahukumiwa. Video iliyorushwa siku ya Jumapili jioni inathibitisha Bw. Faye kama mgombea urais kwa tiketi ya chama cha PASTEF, ambaye ni katibu mkuu.

"Ninamuamini na ninampa nafasi hii," anasema Bw. Sonko. "Bassirou, ni mimi," anaongeza. Anamtambulisha Bw. Faye kama "kaka yake mdogo". "Bassirou ni mwaminifu kama mimi. Bassirou ni mtu mwenye kipaji kikubwa," anabainisha. Anamtaja kama mtu wa vitendo ambaye "amekuwa sehemu ya mradi tangu mwanzo".

"Lazima Bassirou aachiliwe" kwa jina la kanuni ya usawa kati ya wagombea, anasema Bw. Sonko. Kwa upande mwingine, anatoa wito kwa wale ambao wametengwa katika uchaguzi huo kuandamana nyuma ya Bw. Faye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.