Pata taarifa kuu

Ufaransa yavunja kambi ya waomba hifadhi Mayotte

Kuvunjwa kwa kambi ya waomba hifadhi, iliyokumbwa na makabiliano ya hivi majuzi kati ya wakaazi na wakimbizi, kulianza Alhamisi katika wilaya ya mji wa Mamoudzou kwenye kisiwa cha Mayotte, visiwa vya Ufaransa katika Bahari ya Hindi, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu waomba hifadhi kadhaa.

Wimbi jipya la waliowasili mnamo Januari 13 na 14 lilisababisha makabiliano kati ya waomba hifadhi na wakaazi ambao walijaribu kuwazuia kuingia uwanjani, na polisi kulazimika kuingilia kati.
Wimbi jipya la waliowasili mnamo Januari 13 na 14 lilisababisha makabiliano kati ya waomba hifadhi na wakaazi ambao walijaribu kuwazuia kuingia uwanjani, na polisi kulazimika kuingilia kati. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mamia kadhaa ya waomba hifadhi kutoka Afrika, hasa kutoka nchi za Maziwa Makuu, wamewekwa kwa miezi kadhaa katika uwanja wa michezo wa Cavani na katika mitaa iliyokaribu, katika vibanda vilivyotengenezwa kwa mbao na kufunikwa na turubai. Uvunjaji huo ulianza Alhamisi asubuhi, kulingana na vyanzo kadhaa.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Gérald Darmanin, alitangaza kuvunjwa kwa kambi hiyo mnamo Januari 17, kando ya ziara yake katika kisiwa cha Reunion baada ya kupita kwa kimbunga Belal, akibainisha kuwa karibu watu arobaini "ambao wanatambuliwa kama wakimbizi, ambao wana hifadhi" , walirudishwa kutoka nchini Ufaransa. Siku ya Jumatano, Waziri Mkuu, Gabriel Attal, naye alihakikishia Bunge la Seneti kwamba kambi hiyo itavunjwa kuanzia Alhamisi, ahadi ambayo tayari imetolewa na Thierry Suquet, gavana wa Mayotte.

Wimbi jipya la waliowasili mnamo Januari 13 na 14 lilisababisha makabiliano kati ya waomba hifadhi na wakaazi ambao walijaribu kuwazuia kuingia uwanjani, na polisi kulazimika kuingilia kati.

Wakati huo huo, makundi ya wananchi yalikuwa yamefunga kumbi za miji na ofisi za serikali kupinga ujio mkubwa wa wahamiaji katika kisiwa hiki kilicho chini ya mamlaka ya Ufaransa chenye wakaazi wapatao 310,000 kiilichoko katika Bahari ya Hindi. Tangu siku ya Jumatatu, hughuli katika kisiwa hicho zimezorota kutokana  na vizuizi vya barabarani.

Wakimbizi wa kwanza - kutoka Kongo, Rwanda, Burundi au Somalia - walifika "mwanzoni mwa mwaka 2022", Gilles Foucaud, naibu mkurugenzi wa shirika la Solidarité Mayotte, ameliambia shirika la habari la AFP. Lakini tangu mwisho wa mwezi wa Novemba 2023, idadi yao iliongezeka, Jumuiya ya Wananchi ya Mayotte 2018, ambayo inapambana hasa dhidi ya uhamiaji na inashutumiwa na baadhi ya mashirika ya kiutu kwa msimamo unaochukuliwa kuwa wa chuki dhidi ya wageni.

Mnamo 2023, zaidi ya wahamiaji 2,000 wa Kiafrika walipelekwa Mayotte na mitandao haramu ya wasafiri, imebaini halmashauri ya mkoa huo, ambayo ilihalalisha uhamishaji huu na "vipindi kadhaa vya vurugu kati ya wahalifu na wakaazi wa kambi hiyo".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.