Pata taarifa kuu

Watu kadhaa wauawa baada ya jeshi la FARDC kurusha mabomu katika mji wa Mweso

Kitendo cha jeshi la DRC, FARDC, kurusha mabomu na kufyatua risasi katika maeneo yenye watu wengi siku ya Jumatatu katika mji wa Mweso unaodhibitiwa na waasi wa M23, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kilisababisha mtu mmoja kufariki na mmoja kujeruhiwa, vyanzo vya ndani imesema siku ya Jumanne.

Maeneo mawili ya mkoa wa Kivu Kaskazini yamekumbwa na mzozo tangu mwisho wa 2021 ambao unawahusisha M23, wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda, dhidi ya jeshi la Kongo, linalosaidiwa na makundi yenye silaha na makampuni mawili ya kijeshi ya kigeni.
Maeneo mawili ya mkoa wa Kivu Kaskazini yamekumbwa na mzozo tangu mwisho wa 2021 ambao unawahusisha M23, wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda, dhidi ya jeshi la Kongo, linalosaidiwa na makundi yenye silaha na makampuni mawili ya kijeshi ya kigeni. © Alexis Huguet, AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, ullibaini siku ya Jumatatu jioni katika taarifa ya hali ya ndani kwamba "M23 wamezuia wakazi wa Mweso kuelekea maeneo salama", na kwamba mbinu hii ya waasi "innalenga kutumia raia kama ngao za kibinadamu kwa kutarajia mashambulizi yanayoweza kuendeshwa" na jeshi la DRC (FARDC).

Sik ya Jumatatu, karibu tisa alaasiri (saa za Afrika ya Kati), "'mabomu' matatu yalianguka Mweso", yapata kilomita sitini kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, mwanachama wa mashirika ya kiraia amelielezea kwa sharti la kutotajwa jina shirika la habari la AFP. 

Nyumba iliharibiwa na mabomu yaliyorushwa "na FARDC (Jeshi la DRC) kutoka Katsiru (kilomita 7 mashariki mwa Mweso)" na "mtoto alikufa papo hapo", amesema. Siku ya Jumanne mfanyakazi katika hospitali ya Mweso amethibitisha kifo cha "mtoto" na kuongeza kuwa "mwanamke mjamzito alijeruhiwa kwenye paja" wakati wa tukio hilo.

Huko Katsiru, wakaazi wamesema kwamba makombora yalirushwa "kutoka kambi ya FARDC" karibu na kijiji, kilichoko katika sehemu "inayojulikana kama 'Gaza'", na kwamba mabomu hayo yalirushwa kwa minajili ya kuunga mkono shambulio la wanamgambo wanaounga mkono serikali dhidi ya maeneo yanayodhibitiwa na M23 karibu na Mweso. Siku ya Jumanne, hali ya utulivu imerejea Mweso, kulingana na mashahidi kadhaa katika mji huo.

Msemaji wa M23 ameiandika kwenye ukurasa wa mtandao wa X kwamba "majeshi ya muungano wa serikali ya Kinshasa" yametumia "mizinga mizito na () ndege zisizo na rubani" dhidi ya "maeneo yenye watu wengi huko Mweso na viuna vyyake". Kundi hili la waasi linaripoti vifo vya watu wenye umri wa miaka 15 na "watu watatu waliojeruhiwa vibaya". Jeshi lilikuwa bado halijatoa taarifa kuhusu tukio hili siku ya Jumanne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.