Pata taarifa kuu

Misri kusimama na Somalia kuhusu suala la Somaliland

Nairobi – Rais wa Misri, Abdel Fattah al Sisi, amesema kuwa nchi yake haitaruhusu mtu yeyote kutishia uhuru wa Somalia, kufuatia mkataba wenye utata kuhusu matumizi ya bahari ya shamu kati ya hasimu wake Ethiopia eneo lililojitenga na Somalia, la Somaliland.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi
Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi AP - Mandel Ngan
Matangazo ya kibiashara

Katika kikao na waandishi wa habari wakati wa ziara ya rais wa Somalia, Hassan Sheikh mahamud jijini Cairo, Sisi amesisitiza msimamo wa nchi yake kupinga mkataba huo anaosema unakiuka uhuru wa Somalia.

Mvutano wa kikanda umeendelea kuongezeka tangu kutiwa saini kwa mkataba wa maelewano kati ya Ethiopia na Somaliland Januari mosi, wiki iliopita, waziri wa mambo ya nje wa Misri, akiitaja Ethiopia kama chanzo cha ukosefu wa utulivu.

Mogadishu kwa upande wake imeendelea kukashifu mkataba huo na kuutaja kama kitendo cha uchokozi, huku ikipuzilia mabali uwezekano wa kuwepo mazungumzo hadi pale Ethiopia itakapofuta mkataba wake na Somaliland.

Utawala wa Adiss Ababa na cairo umekuwa kwenye mvutano kwa miaka mingi, hasa kuhusu bwawa kubwa la kuzalisha umeme la Ethiopia ambao Cairo inasema linatishia usalama wake wa maji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.