Pata taarifa kuu

Sudan 'yasimamisha' uhusiano wake na IGAD, muungano wa Afrika Mashariki

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan, tiifu kwa jeshi la Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, imetangaza siku ya Jumanne "kusimamisha" uhusiano wake na IGAD, kambi ya kikanda ya Afrika Mashariki, inayotuhumiwa "kukiuka uhuru wa Sudan.

Kwa miezi kadhaa, jeshi na serikali ya Sudan vimeendelea kushutumu "upendeleo" wa kambi ya kikanda na nchi za Afrika Mashariki.
Kwa miezi kadhaa, jeshi na serikali ya Sudan vimeendelea kushutumu "upendeleo" wa kambi ya kikanda na nchi za Afrika Mashariki. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wizara ya Mambo ya Nje imefahamisha (...) IGAD juu ya uamuzi wa Sudan wa kuacha kushirikiana na kusimamisha uhusiano wake" na jumuiya hiyo ya kikanda, inabainisha taarifa kutoka wizara ambayo inaishutumu "kukiuka uhuru wa Sudan.

Tangu Aprili 15, jeshi na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) vya Jenerali Mohammed Hamdane Daglo vimekuwa katika vita vya kuwania madaraka nchini Sudan. Mgogoro huu umesababisha vifo vya zaidi ya watu 13,000, kulingana na makadirio ya sirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED). Kwa kuongezea, zaidi ya watu milioni saba wamelazimika kuyahama makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Mkuu wa FSR, mpinzani wa Jenerali Burhane, ameongeza safari zake barani Afrika katika wiki za hivi karibuni, na alialikwa na IGAD kwenye mkutano wa Alhamisi huko Kampala, nchini Uganda.

"Kualika kiongozi wa wanamgambo" FSR ni "mfano hatari" na "inakiuka katiba ya IGAD," wizara imeongeza. Kwa miezi kadhaa, jeshi na serikali ya Sudan imeendelea kushutumu "upendeleo" wa kambi ya kikanda na nchi za Afrika Mashariki.

Juhudi za kidiplomasia za mazungumzo ya amani, hasa na Marekani, Saudi Arabia na, hivi karibuni, IGAD, hadi sasa zimeshindwa. Majenerali Burhane na Daglo walikuwa wameungana hapo awali kutekeleza uvamizi na kuwaondoa raia madarakani mnamo Oktoba 2021, na hivyo kuhitimisha miaka miwili ya mpito wa kidemokrasia.

kambi zote mbili ambazo hazijaweza kushinda cita hivi tangu kuanza kwa vita, zimekwama lakini hakuna nia ya kufanya makubaliano yoyote kwenye meza ya mazungumzo. Hata hivyo, kimsingi FSR inaonekana kupata maeneo mapya katika uso wa upinzani dhaifu kutoka kwa jeshi. Sasa wanadhibiti mitaa ya Khartoum, karibu eneo lote la magharibi mwa Darfur na wameingia katika jimbo la al-Jazeera, mashariki mwa kati mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.