Pata taarifa kuu

WHO imeeleza kuguswa na hali mbaya ya afya nchini Ethiopia

Nairobi – Shirika la afya duniani, limeeleza kuguswa na hali mbaya ya afya nchini Ethiopia, huku ukame, mapigano na mamia ya watu kukimbia makazi yao, vikichangia ongezeko la magonjwa na njaa.

Watoto wanakabiiwa na utapia mlo kwa ukosefu wa chazkula chenye madini hali ambayo inahatarisha maisha yao
Watoto wanakabiiwa na utapia mlo kwa ukosefu wa chazkula chenye madini hali ambayo inahatarisha maisha yao AP - Martial Trezzina
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya pamoja ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Ethiopia na Mamlaka inayoshughulikia majanga nchini humo inasema watu wanaoishi kwenue majimbo ya Afar, Amhara, Tigray na Oromia ndio waliothiriwa zaidi.

Ukame umesababisha kushuka kwa uzalishaji wa kilimo na kupatikana kwa chakula na kuwaacha mamilioni ya watu bila chakula, kutokana na uhaba wa mvua.

Watoto wanakabiiwa na utapia mlo kwa ukosefu wa chazkula chenye madini hali ambayo inahatarisha maisha yao.

Aidha, maeneo hayo yanakabiiwa na uhaba wa maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na wanyama, hali inayotishia watu kusumbuliwa na magonjwa yanayoletwa a matumizi ya maji chafu.

Kati ya mwezi Julai na Desemba mwaka 2023, watu Milioni 7.3 walipokea msaada wa chakula kutoka mashirika yanyatoa misaada likiwemo lile la mpanfo wa chakula dunini WFP na msaadfa hauo hautoshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.