Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-SIASA

Niger: Waziri Mkuu anaomba kuahirishwa kwa mkutano uliopangwa kufanyika Januari 10 na ECOWAS

Mkutano wa kuendeleza mazungumzo uliopangwa kufanyika siku ya Jumatano Januari 10, 2024 mjini Niamey kati ya ujumbe wa upatanishi wa ECOWAS na Niger hautafanyika tena. Katika barua rasmi ambayo RFI ilipata nakala yake, Waziri Mkuu wa Niger anaomba kuahirishwa kwa mkutano huu hadi Januari 25 ili kutoa muda kwautawala wa kijeshi wa Niger kuandaa Kongamano la Kitaifa la Mazungumzo.

Ali Mahamane Lamine Zeine Niger
Katika barua rasmi, Waziri Mkuu wa Niger Ali Mahamane Lamine Zeine (picha yetu) anaomba kuahirishwa kwa mkutano na ECOWAS hadi Januari 25 ili kutoa muda kwa utawala wa kijeshi wa Niger kuandaa kongamano la kitaifa la mazungumzo. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Uamuzi huu wa serikali ya Niger unaweza kuelezewa kama "mabadiliko ya kauli".

Mwezi uliopita wakati wa ziara ya kwanza ya Niamey, ujumbe kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi uliridhika. Majadiliano ya kwanza hasa yalihusu muda wa mpito.

Baada ya mazungumzo ya kitaifa

Mwishoni mwa vikao, wajumbe wa ECOWAS walitangaza rasmi: "Tumekubaliana juu ya maudhui na wakati wa mpito". Baada ya kuripoti majadiliano ya vikao vyao na Niamey kwa Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, rais wa sasa wa ECOWAS, wajumbe hawa walipaswa kurejea Niger siku ya Jumatano kuendelea na majadiliano. Hatimaye, watasubiri kongamano la kitaifa litakalofanyika nchini Niger.

"Hivi ndivyo vikosi vimeamua"

Wakati wa mkutano huu, ambao unakusudiwa kujumuisha wadau wote lakini ambao kwa uhalisia utadhibitiwa kwa uangalifu na utawala wa kijeshi, muda wa mpito na majukumu ya kukamilishwa kabla ya kuandaa chaguzi zinazowezekana kubainishwa. Sasa ni baada ya kazi hii ambapo Niamey inataka kukutana na ujumbe wa ECOWAS ili pengine kuiambia: "Hivi ndivyo vikosi vimeamua".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.