Pata taarifa kuu

Misri inasimama na Somalia: Rais Fattah al-Sisi

Nairobi – Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi, ameahidi kusimama na nchi ya Somalia katika mzozo wake na Ethiopia kuhusu makubaliano kuhusu matumizi ya Bahari Nyekundu na Somaliliand.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka wa 1991 japokuwa haijatambuliwa kimataifa kama nchi huru
Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka wa 1991 japokuwa haijatambuliwa kimataifa kama nchi huru AP - Mandel Ngan
Matangazo ya kibiashara

Ethiopia na jimbo linalojitawala la Somaliland, lililotangaza kujitenga na Somalia mwaka 1991, zilitia saini mkataba wa ushirikiano ambao, wachambuzi wanasema huenda ukazua mzozo katika ukanda wa pembe ya Afrika.

Somalia, ambayo inasema Somaliland ni sehemu yake, imekashifu makubaliano hayo ikisema ni ya kichokozi na hayana msingi wa kisheria.

Somaliland ilijitenga na Somalia mwaka wa 1991 japokuwa haijatambuliwa kimataifa kama nchi huru.

Katika mazungumzo ya njia ya simu na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, Rais Sisi aliahidi msimamo wa nchi yake na Somalia na kwamba Misri inaiunga Mogadishu mkono katika masuala ya kiusalama na uthabiti.

Somalia imesema itatumia mbinu zote za kisheria kulinda himaya yake
Somalia imesema itatumia mbinu zote za kisheria kulinda himaya yake AP - Evelyn Hockstein

Kando na suala la Somaliland, msemaji wa rais Sisi Ahmed Famy, aliongeza kuwa viongozi hao pia walijadili maendeleo ya ukanda na ushirikiano.

Rais Mohamud pia alifanya mazungumzo na Emir wa Qatar Tamim bin Hamad kuhusiana na ushirikiano, kwa mujibu wa afisi ya rais wa Somalia.

Katika hatua nyingine, Umoja wa Ulaya umesisitiza kuheshimiwa kwa uhuru wa nchi Somalia na nchi jirani ya Ethiopia.

EU katika taarifa yake imetaka Ethiopia kuheshimu mikataba ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuhusu uhuru wa nchi nyingine, ili kuendelea kudumisha usalama na amani ya kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.