Pata taarifa kuu

Ethiopia: Serikali imekanusha kuwa eneo la Tigray linakabiliwa na njaa

Nairobi – Serikali ya Ethiopia imekanusha onyo la uongozi wa jimbo la Tigray, kuwa linakabiliwa na ukame baada ya vita vya miaka miwili. 

Serikali ya Ethiopia imekanusha onyo la uongozi wa jimbo la Tigray, kuwa linakabiliwa na ukame baada ya vita vya miaka miwili
Serikali ya Ethiopia imekanusha onyo la uongozi wa jimbo la Tigray, kuwa linakabiliwa na ukame baada ya vita vya miaka miwili AP
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa, Getachew Reda, rais wa mpito wa jimbo la Tigray, amesema eneo hilo linakumbwa na baa la njaa na watu wengi wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha. 

Reda, amefananisha hali inayoendelea kama ile iliyoshuhudiwa wakati wa miaka 1980 wakati watu zaidi ya Milioni moja walipopoteza maisha. 

Hata hivyo, msemaji wa serikali, Legesse Tulu, amekanusha ripoti za uongozi wa Tigray, lakini akakiri kuwa ni kweli mamilioni ya watu wanakabiliwa na ukame na mafuriko. 

Vita kati ya waasi wa Tigray na wanajeshi wa serikali, vilianza Novemba mwaka 2020 na kusababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na kuwaacha wengine zaidi ya Milioni moja wakiyakimba makaazi yao. 

Mwezi Juni, Shirika la misaada la Marekani USAID na Shirika la Mpango wa Chakula duniani, walisitisha msaada wa chakula nchini Ethiopia, kwa madai kuwa msaada huo ulikuwa unaibiwa. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.