Pata taarifa kuu

Safari za misaada ya kibinadamu za Umoja wa Mataifa zatishia kusitishwa nchini Niger

Safari za ndege za misaada ya kibinadamu za Umoja wa Mataifa kuelekea Niger zinaweza kusitishwa mapema mwezi Februari kutokana na ukosefu wa fedha, katika nchi hii inayotawaliwa na jeshi tangu mapinduzi ya mwezi Julai, ambapo watu milioni 4.3 wanahitaji msaada, limetangaza shirika la kimataifa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP.

Tangu mapinduzi hayo, Niger inakabiliwa na vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).
Tangu mapinduzi hayo, Niger inakabiliwa na vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). AFP - HANDOUT
Matangazo ya kibiashara

"Huduma ya Umoja wa Mataifa ya Kuhudumia Misaada ya Kibinadamu (UNHAS), inayosimamiwa na WFP (...) inaweza kusitishwa mara moja kutokana na ukosefu wa fedha," imeandika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) na WFP katika taarifa ya pamoja.

Bajeti ya UNHAS "inafikia dola milioni 13.5 kwa 2024 lakini bila dhamana yoyote ya ufadhili hadi sasa, wakati nusu ya kiasi hiki inahitajika haraka", kulingana na chanzo hicho.

"Hali ya kifedha ya UNHAS tayari inatulazimisha kupunguza safari zake hadi ndege moja ikilinganishwa na mbili za sasa, ili kupunguza gharama zake za uendeshaji mara moja, lakini bila kuathiri vibaya shughuli za kibinadamu," alisema mwakilishi na mkurugenzi wa WFP katika nchi ya Niger, Jean-Noël Gentile, akinukuliwa katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Uwezo wa uokoaji wa matibabu" "utaathirika sana", OCHA na WFP wameongeza.

Kulingana na Bw. Gentile, "bila ufadhili wa ziada wa haraka, huduma nzima ya UNHAS italazimika kusitishwa kuanzia mwezi wa Februari 2024".

Umoja wa Mataifa ulitangaza kuanza tena kwa safari zake za ndege za kibinadamu katikati ya mwezi wa Novemba, zilizositishwa baada ya mapinduzi ya Julai 26 ya wanajeshi walio madarakani.

Shirika la kimataifa, hata hivyo, liliweza kuendelea na usaidizi wake vinginevyo na katika baadhi ya maeneo tu ya nchi hii kubwa ya jangwa ambapo watu milioni 4.3 wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Mnamo Oktoba, majenerali wa Niger pia waliagiza kufukuzwa kwa mratibu wa Umoja wa Mataifa katika nchi hii, Louise Aubin.

Tangu mapinduzi hayo, Niger inakabiliwa na vikwazo vizito vya kiuchumi na kifedha vilivyowekwa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.