Pata taarifa kuu

Kifaransa si lugha ya taifa tena nchini Burkina Faso

Serikali ya Burkina Faso ilipitisha siku ya Jumatano mswada wa kurekebisha Katiba na kuanzia sasa kuweka lugha za taifa kama lugha rasmi badala ya Kifaransa ambacho kimeshushwa kwenye daraja la "lugha ya kazi".

Maandamano ya kuunga mkono jeshi, mwaka mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi huko Ouagadougou.
Maandamano ya kuunga mkono jeshi, mwaka mmoja baada ya mapinduzi ya kijeshi huko Ouagadougou. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Baraza la Mawaziri inabainisha kwamba muswada huu "ni sehemu ya utekelezaji wa moja ya dhamira kuu za mpito ambayo inajumuisha kuanzisha mageuzi ya kisiasa, kiutawala na kitaasisi kwa nia ya kuimarisha utamaduni wa kidemokrasia na kuunganisha utawala wa sheria." . Miongoni mwa "ubunifu mkubwa" wa nakala hii mpya ni "kuanzishwa kwa lugha za taifa kama lugha rasmi badala ya Kifaransa ambacho kinakuwa lugha ya kazi".

Mapema mwaka huu, Mali, inayotawaliwa na jeshi kama Burkina na ambayo pia ina uhusiano mbaya na Ufaransa, ilirekebisha Katiba yake kwa kura ya maoni na kuwawekea Wafaransa hatima hiyo. Mswada huu, ambao bado utapigiwa kura na Bunge la Mpito, pia unatoa nafasi ya "kuanzishwa kwa mbinu za jadi na mbadala za kutatua migogoro".

Baraza la Katiba linaona majukumu yake yakipanuliwa huku taasisi zikifutwa kama vile Mahakama Kuu ya Haki iliyohukumu viongozi wakuu wa kisiasa au Mpatanishi wa Faso. Hatimaye, idara ya ujasusi (ANR) inaona hadhi yake ikiimarishwa kwa sasa kulindwa katika Katiba.

Katika miezi ya hivi karibuni, maandamano kadhaa ya kupitishwa kwa Katiba mpya yalifanyika nchini. Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye aliingia madarakani Septemba 2022, aliahidi marekebisho ya sehemu ya Katiba miezi miwili iliyopita.

"Kuandikwa kwa Katiba mpya ni suala la uhuru wa kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Hakuna mtu anayeweza kustawi kutokana na dhana za wengine," Waziri Mkuu Apollinaire Joachimson Kyelem wa Tambela alitangaza siku ya Ijumaa, akirejea kwenye bakala iliyoigwa kwenye katiba ya Ufaransa. 

Tangu Kapteni Traoré aingie madarakani, Burkina Fso imejitenga na Ufaransa, mkoloni wa zamani na mshirika wa kihistoria, huku ikiimarisha uhusiano wake na Moscow. Tangu mwaka 2015, Burkina imekumbwa na msururu wa ghasia zinazofanywa na makundi ya wanajihadi, ambayo tayari yalikuwa yakishambulia nchi jirani za Mali na Niger na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 17,000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.