Pata taarifa kuu

Ujumbe wa Urusi nchini Niger ili kuimarisha ushirikiano wa kijeshi

Ujumbe wa Urusi ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi umewasili Niamey ili kujadiliana na mamlaka ya kijeshi, ambao waliingia madarakani kupitia mapinduzi mwishoni mwa mwezi wa Julai, utawala wa kijeshi umetangaza Jumatatu kwenye redio ya kitaifa.

Mmoja wa waandamanaji wanaounga mkono jeshi la Jenerali Tiani akipeperusha bendera ya Urusi mjini Niamey Julai 2023.
Mmoja wa waandamanaji wanaounga mkono jeshi la Jenerali Tiani akipeperusha bendera ya Urusi mjini Niamey Julai 2023. © AP
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza rasmi kwa mjumbe wa serikali ya Urusi nchini humo tangu mapinduzi ya Julai 26 ambayo yalivuruga uhusiano wa kidiplomasia kati ya Niger na washirika wake wa kimataifa.

Ujumbe huo ukiongozwa na Naibu Waziri wa Ulinzi wa Urusi, Kanali Jenerali Yunus-Bek Yevkurov, umepokelewa Jumatatu na mkuu wa utawala wa kijeshi wa Niger, Jenerali Abdourahamane Tiani. Mwishoni mwa mkutano huu, wahusika waliendelea "kutia saini hati kama sehemu ya uimarishaji wa ushirikiano wa kijeshi kati ya Jamhuri ya Niger na Shirikisho la Urusi", imebainisha mamlaka ya Niger.

Diplomasia ya Urusi inajikuta katika nafasi nzuri nchini Niger wakati Ufaransa, mshirika wa karibu wa serikali iliyotimuliwa madarakani, imekuwa ikilengwa na mamlaka mpya ambayo imelaani mikataba ya ushirikiano na kuitaka Ufaransa kuondoa wanajeshi wake 1,500 waliotumwa katika nchi hii inayokumbwa na vurugu za wanajihadi.

Ujumbe huu wa Urusi ulikwenda Jumapili Bamako nchini Mali, mshirika wake mkuu katika eneo hilo, ambalo pia linatawaliwa na jeshi.

Majadiliano hayo yalihusu hasa "miradi ya maendeleo ya Mali, katika suala la nishati mbadala na nishati ya nyuklia", pamoja na "maswali yanayohusiana na usambazaji wa mbolea, ngano na bidhaa za petroli nchini Mali", amebainisha Aousséni Sanou, Waziri wa Uchumi na Fedha wa Mali, katika video iliyochapishwa na ofisi ya rais.

Pia ametaja ujenzi wa reli na njia ya treni za mwendo kasi, kuundwa kwa shirika la ndege la kikanda, pamoja na miradi ya utafiti na uchimbaji madini.

Tawala za kijeshi za Mali, Niger na Burkina Faso, nchi za Saheli zilizoathiriwa zaidi na ghasia za wanajihadi na ambazo uhusiano wao na Ufaransa ni mbaya, wamekutana katika wiki za hivi karibuni na kuunda Muungano wa Mataifa ya Sahel.

Siku ya Jumamosi, Burkina Faso na Niger zilitangaza, kama Mali mnamo 2022, wamejiondoka katika kundi la nchi za G5 Sahel zinazopambana na wanajihadi, linaloungwa mkono na washirika wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.