Pata taarifa kuu

Wahamiaji wanne wa Morocco wamefariki pwani ya Uhispania

Wahamiaji wanne wa Morocco wamefariki kusini mwa mji Cadiz, pwani ya Uhispania, wengine wanne wakipelekwa hosipitalini kupokea matibabu baada ya kuathiriwa na viwango vya juu vya baridi.

Wahamiaji kutoka barani Afrika wamekuwa wakitumia njia ya Uhispania kuingia Ulaya
Wahamiaji kutoka barani Afrika wamekuwa wakitumia njia ya Uhispania kuingia Ulaya © Europa Press via AP
Matangazo ya kibiashara

Miili ya wanne hao ambao inaaminika kuwa walizama, ilipatikana siku ya Jumatano karibu na boti lao ambalo lilikuwa likiwasafirisha wahamiaji wengine 32.

Kwa mujibu wa taarifa, wahamiaji 27 waliokuwa kwenye boti hilo, walilazimishwa kuruka baharini na wahudumu wa chombo hicho ambapo 23 kati yao waliokolewa wakiwa hai. Tayari polisi wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Mamia ya wahamiaji wamekuwa wakitumia njia hatari kuingia barani Ulaya
Mamia ya wahamiaji wamekuwa wakitumia njia hatari kuingia barani Ulaya AP

Naibu rais wa Uhispania ambaye pia ndiye waziri wa leba Yolanda Diaz, amethibitisha kupokea taarifa kuhusu tukio hilo.

Mamia ya raia kutoka barani Afrika wamekuwa wakiendelea kutumia njia hatari za usafiri wa baharini wakiwa na lengo la kuingia barani Ulaya kutafuta maisha bora.

Katika taarifa yake, Yolanda Diaz ameutaka Umoja wa Ulaya kuchukua hatua dhidi ya kuzuia na kudhibiti ongezeko la wahamiaji.

Mifano ya boti ambazo wahamiaji wamekuwa wakitumia kuingia barani barani
Mifano ya boti ambazo wahamiaji wamekuwa wakitumia kuingia barani barani AP - Felipe Dana

Uhispania ndiyo njia kuu ya wahamiaji kutoka Afrika Kaskazini kuingia barani Ulaya, Makumi kwa maelfu ya wahamiaji wakithibitishwa kuwasili kwenye eneo hilo mwaka uliopita peke.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.