Pata taarifa kuu

Kenya: Serikali imeweka mikakati kukabiliana na athari za mafuriko

Rais wa Kenya William Ruto amesema serikali yake imeweka mipango ya kuwasaidia raia wake ambao wameathirika na mafuriko yanayoendelea kuripotiwa kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki.

Serikali ya Kenya inasema imeweka mikakati kukabiliana na athari za mafuriko
Serikali ya Kenya inasema imeweka mikakati kukabiliana na athari za mafuriko © State House Kenya
Matangazo ya kibiashara

Rais Ruto amekutana hii leo Jumamosi na idara mbalimbali zinazohusika na kukabiliana na majanga katika Ikulu ya Nairobi ambapo amethibitisha kuwa karibia watu 70 wamefariki katika mafuriko hayo wakati wengine elfu 36 wakipoteza makazi yao baada ya nyumba zao kufirika.

Aidha mkuu wa nchi ameonya kuwa mvua itaendelea kunyesha ambapo maandalizi zaidi yanahitajika kukabiliana na dharura zinazoweza kutokea.

Kutokana na hali inayoendelea kushuhudiwa kwa sasa, baraza la mawaziri linatarajiwa kukutana siku ya Jumatatu ambapo suala la mafuriko linatarajiwa kujadiliwa kwa mujibu wa wachambuzi wa mambo.

Rais Ruto amethibitisha kuwa karibia watu 70 wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo
Rais Ruto amethibitisha kuwa karibia watu 70 wameripotiwa kufariki katika mafuriko hayo © State House Kenya

Kikao hicho aidha kinatarajiwa kujadili mbinu muafaka zinazohitajika kukabiliana na athari zinazotokana na mafuriko ambayo yameendelea kuwa changamoto kwa raia katika taifa hilo la Afrika.

Mkuu wa nchi aidha ameeleza kuwa nchi iko katika sehemu nzuri ya kukabiliana na athari za mafuriko haswa wakati huu serikali kuu inaposhirikiana na zile za majimbo.

Wanajeshi kutumika kupeleka misaada katika maeneo ambayo yamefurika zaidi kutokana na mafuriko
Wanajeshi kutumika kupeleka misaada katika maeneo ambayo yamefurika zaidi kutokana na mafuriko © State House Kenya

Rais Ruto vilevile amesema kuwa wanajeshi watasaidia katika upelekaji wa misaada katika maeneo yaliombali na ambayo yamefunikwa na mafuriko ambapo pia vitengo vingine wa walinda amani vitatumika kuhakikisha usalama wa raia.

Kando na hayo, Rais Ruto ametoa wito kwa raia wake kutumia mvua inayoendelea kunyesha kuboresha na kujiunga katika kilimo.

Mataifa ya Pembe ya Afrika yanakabiliwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha, nchi za Kenya na Somalia zikiripoti maafa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.