Pata taarifa kuu

EAC: Nchi wanachama kuongoza vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa: Rais Ruto

Rais wa Kenya, William Ruto amesema ni lazima hatua za kiubunifu na endelevu zibuniwe ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Rais wa Kenya William Ruto amesema EAC itaongoza katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa
Rais wa Kenya William Ruto amesema EAC itaongoza katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa © State House Kenya
Matangazo ya kibiashara

Hatua ambazo rais Ruto amesema zitachukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ikielekea Dubai kwa mkutano kuhusu mazingira wa COP28 baadaye mwezi huu.

Akizungumza katika kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula jijini Arusha, Rais Ruto amemsea Afrika itatumia na kuonyesha uwezo wake katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Mkutano wa EAC kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula unafanyika nchini Tanzania
Mkutano wa EAC kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula unafanyika nchini Tanzania © State House Kenya

Miongoni mwa viongozi wa nchi za EAC wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Evariste Ndayishimiye (Burundi) na Salva Kiir (Sudan Kusini).

Miongoni mwa viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na waziri mkuu wa Rwanda Edouardo Ngirente Rebecca Kadaga, naibu waziri mkuu wa kwanza wa Uganda.

Mataifa ya pembe ya Afrika ikiwemo Kenya na Somalia kwa sasa yanakabiliwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha
Mataifa ya pembe ya Afrika ikiwemo Kenya na Somalia kwa sasa yanakabiliwa na mafuriko yanayosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha © State House Kenya

Aidha rais Ruto ameeleza kuwa Afrika itatoa wito wa kusainiwa kwa mkataba mpya wa ufadhili ambao utarekebisha mfumo wa sasa wa kifedha wa kimataifa, ambao hauendani na hali ya sasa ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kenya, EAC na Afrika, alieleza, zinajenga muungano wa kimataifa utakaosaidia kuipa dunia mtazamo mapya ambayo utasaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Viongozi wengine wanaohuduria kikao hicho ni pamoja na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Burundi, Evariste Ndayishimiye
Viongozi wengine wanaohuduria kikao hicho ni pamoja na rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na mwenzake wa Burundi, Evariste Ndayishimiye © State House Kenya
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.