Pata taarifa kuu

Bamako kujenga kiwanda cha kusafisha dhahabu

Serikali ya kijeshi nchini Mali, imetia saini makubaliano kuhusu mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha dhahabu katika jiji kuu la Bamako kati yake na nchi ya Urusi.

Mkataba huo unajumuisha ujenzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kusafisha tani 200 za dhahabu kila mwaka
Mkataba huo unajumuisha ujenzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kusafisha tani 200 za dhahabu kila mwaka © RFI
Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo unajumuisha ujenzi wa kiwanda hicho chenye uwezo wa kusafisha tani 200 za dhahabu kila mwaka.

Pande hizo mbili hazijaweka wazi muda ambao mardi huo utakuwa umekamilika japokuwa unatarajiwa kujengwa katika kipindi cha miaka minne.

Dhahabu ndiyo bidhaa inayoongoza nchini Mali kwa thamani ambapo pia inachangia wachangiaji kwa sehemu kubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo, kulingana na wizara ya madini ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa  waziri wa fedha wa Mali, Alousséni Sanou, mradi huo utaipa nchi yake uwezo wa kudhibiti uzalishaji wote wa dhahabu.

Mali imeimarisha uhusiano wake na Urusi katika miaka ya hivi karibuni kufuatia mapinduzi ya kijeshi mwaka 2021 na kuondolewa kwa vikosi vya Ufaransa nchini humo mwaka mmoja baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.