Pata taarifa kuu

Wataalam waonya kuhusu uwezekano wa kilichotokea Libya kutokea Sudan

Ikiwa ni takribani miezi 7 tangu vita vianze nchini Sudan na kusababisha vifo vya maelfu ya raia na mamilioni wengine kukimbia makazi yao, wataalamu wameonya kuwa huenda taifa hilo likasambaratika kama kilichotokea nchini Libya.

Onyo lao limekuja wakati huu Jumuiya ya kimataifa ikijaribu kuongeza shinikizo kwa jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, kusitisha mapigano
Onyo lao limekuja wakati huu Jumuiya ya kimataifa ikijaribu kuongeza shinikizo kwa jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, kusitisha mapigano © AFP
Matangazo ya kibiashara

Onyo lao limekuja wakati huu Jumuiya ya kimataifa ikijaribu kuongeza shinikizo kwa jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, kusitisha mapigano.

Licha ya wito wa kusitishwa kwa mapigano kutoka kwa Jumiya ya kimataifa, pande hasimu kwenye taifa hilo zimeendelea kukabiliana katika maeneo tofauti, kila upande ukiituhumu mwengine kwa kuanzisha mashambulio.

Maelfu ya raia wametoroka makazi yao kutokana vita vinavyoendelea kati ya RSF na jeshi la serikali
Maelfu ya raia wametoroka makazi yao kutokana vita vinavyoendelea kati ya RSF na jeshi la serikali AFP - -

Lakini je, suluhu inaweza kupatikana? Hamduni Marcel ni mtaalamu wa siasa za kimataifa anaangazia hili akiwa Tanzania.

‘‘Haiwezekani kupatikana suluhu kama watengenezaji wa fitina hii hawajaamua imemalizike, hilo ni jambo ambalo linastahili kuangaliwa sana.’’ alisema Hamduni Marcel ni mtaalamu wa siasa za kimataifa anaangazia hili akiwa Tanzania.

Maelfu ya raia wa Sudan wametoroka mapigano yao wengi wakipewa hifadhi katika nchi jirani ikiwemo Chad na Sudan Kusini.

Takwimu za mashirika ya kiraia zinaonyesha kuwa mamia ya watu wameuwa katika mapigano hayo yanayoendelea kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la Sudan.

Wataalam wanaonya kuwa huenda kilichotokea nchini Libya kikatokea nchini Sudan
Wataalam wanaonya kuwa huenda kilichotokea nchini Libya kikatokea nchini Sudan © Zohra Bensembra / Reuters

Mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo unaoendelea ambayo yanaoongozwa na Marekani na Saudi Arabia yamekuwa yakiendelea jijini Jeddah yakionekana kutozaa matunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.