Pata taarifa kuu

Afrika : Berlin kuwekeza euro bilioni 4 katika miradi ya nishati mbadala

Nairobi – Ujerumani imesema itawekeza euro bilioni 4 katika miradi ya nishati mbadala barani Afrika hadi mwaka 2030, Kansela Olaf Scholz akisema mpango huu unaweza kuzisaidia nchi za Ulaya kufikia malengo yake kuhusu udhibiti wa Kaboni.

Mkutano huu kati ya nchi za G20 na bara Afrika ulilenga kuongeza uwekezaji katika bara maskini zaidi lakini linalokuwa kwa kasi duniani
Mkutano huu kati ya nchi za G20 na bara Afrika ulilenga kuongeza uwekezaji katika bara maskini zaidi lakini linalokuwa kwa kasi duniani via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Ujerumani itahitaji kuagiza kiasi kikubwa cha hidrojeni kutoka nje, ikiwa ni pamoja na kutoka Afrika, kama inataka kufikia lengo lake la kudhibiti hewa kaa ifikapo mwaka 2045, alisema kansela Scholz wakati wa kongamano la wafanyabiashara wa Ujerumani na Afrika mjini Berlin.

Mkutano huo unafanyika jijini Berlin Ujerumani
Mkutano huo unafanyika jijini Berlin Ujerumani via REUTERS - POOL

Mkutano huu kati ya nchi za G20 na bara Afrika ulilenga kuongeza uwekezaji katika bara maskini zaidi lakini linalokuwa kwa kasi duniani kwa kuratibu ajenda za maendeleo za nchi zinazozingatia mageuzi na kubainisha fursa za biashara.

Euro bilioni 4 zitaelekezwa katika Mpango wa pamoja wa EU na Afrika wa Nishati mbadala, ambapo tayari EU ilikuwa imetangaza kutoa msaada wa euro bilioni 3.4.

Rais wa Comoros , Azali Assoumani, akihudhuria mkutano wa G20 nchini Ujerumani
Rais wa Comoros , Azali Assoumani, akihudhuria mkutano wa G20 nchini Ujerumani AP - Markus Schreiber

Mkutano wa kilele wa Mkataba wa G20 na Afrika hapo jana, ulikuwa wa tano tangu kuundwa kwake mwaka 2017 ambapo viongozi kutoka mataifa 10 ya Afrika walihudhuria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.