Pata taarifa kuu

Kenya: Bei ya mafuta kushuka mwezi Desemba: Rais Ruto

Nairob – Rais wa Kenya William Ruto amesema bei ya mafuta ambayo kwa sasa iko juu, itashuka mwezi Desemba ya mwaka huu.

Baadhi ya raia wamekuwa wakimtuhumu rais Ruto kwa kushindwa kutimiza ahadi zake za wakati wa kampeni
Baadhi ya raia wamekuwa wakimtuhumu rais Ruto kwa kushindwa kutimiza ahadi zake za wakati wa kampeni REUTERS - MONICAH MWANGI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika kaunti ya Kirinyaga katika mkoa wa kati kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki, mkuu wa nchi amesema serikali yake imekuwa ikiangazia namna ya kutatua changamoto zinazowakabili raia ikiwemo kupanda kwa bei ya mafuta.

Raia wa taifa hilo wameendelea kuituhumu serikali kwa kushindwa kutatua tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta, suala ambalo limechangia kupanda kwa bei za bidhaa nyengine ikiwemo chakula.

"Bei ya mafuta sasa tumeanza kushughulikia. Bei ya mafuta imepanda kila mahali lakini kama Kenya tulifanya mpango, tumetafuta namna ya kuhakikisha kwamba bei isipite mahali ambapo Wakenya wengi wataumia," ameeleza rais Ruto.

Raia wa Kenya wamekuwa wakilipa shillingi 217.36 kwa kila lita ya mafuta aina ya petroli, shillingi 205.47 kwa mafuta aina ya dieseli na shillingi 204.46 kwa mafuta taa katika kipindi cha mwezi Oktoba.

Bei za bidhaa ya mafuta aina ya petroli imesalia vilevile katika kipindi cha mwezi Novemba na Desemba wakati ile ya mafuta aina ya diseli na mafuta taa ikipungua kwa shillingi mbili pesa ya taifa hilo.

“Mmeona mwezi huu hio bei imeanza kushuka, mwezi ujao itashuka zaidi.” ameongeza rais Ruto.

Bei hizo za mafuta zitasalia hivyo hadi tarehe 14 ya mwezi Desemba wakati bodi ya kudhibti bei ya kawi nchini humo itakapotangaza bei mpya.

Rais Ruto ameeleza kuwa suala la kupanda kwa bei za mafuta inashuhudiwa duniani kote ila serikali yake inashugulikia namna ya kutatua suala hilo na wale wanaowauzia mafuta.

Kiongozi huyo aidha amewataka raia wa Kenya kuipa serikali yake muda wakati huu anaposhugulikia changamoto zinazoikabili nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.