Kenya: Ruto atambuliwa kwa mchango wake kuhusu mazingira
Nairobi – Rais wa Kenya William Ruto ametambuliwa na Jarida la Time kuwa miongoni wa viongozi 100 wenye ushawishi mkubwa zaidi duniani kutokana na mchangao wao kuhusu kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya rais Ruto kuwaongoza raia wa taifa lake katika zoezi la upanzi wa miche milioni 100 kwa siku moja.
In Kiu, Makueni County, during the #NationalTreePlantingDay. pic.twitter.com/Qick7hi9e1
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) November 13, 2023
Ruto aliteuliwa pamoja na meya wa mji mkuu wa Sierra Leone Freetown, Yvonne Aki-Sawyerr.
Mbunifu mwenye uraia wa Burkina Faso na Ujerumani Francis Kéré na mjasiriamali wa hali ya hewa raia wa Ethiopia Kidus Asfaw pia walitambuliwa.
Orodha hiyo, inayojulikana kama "Time 100 Climate", ilitolewa siku ya Alhamisi, na ni jaribio la uzinduzi wa jarida hilo kutaja wale inaowaona kuwa muhimu katika kuangazia na kufanya jambo kuhusu suala la mabadiliko ya hali ya hewa kote ulimwenguni.
Kwa mujibu wa Time, hatua hiyo iliafikiwa baada ya kuangazia juhudi na maendeleo makubwa yaliopigwa katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Jarida hilo pia lilisema kuwa viongozi hao walichaguliwa kwa sababu ya juhudi zao katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yalikuwa ya hivi karibuni ambapo pia yalitoa mafanikio makubwa yanayoonekana.
Ruto amekuwa amekuwa mstari wa mbele kujaribu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa nchini Kenya na Afrika.
Siku iliyotengwa na serikali kwa lengo la kupanda miche ambayo ilifanyika tarehe 13 Novemba ilikuwa sehemu ya azma yake kubwa kwa Kenya kupanda miti bilioni 15 katika miaka 10.
Mnamo Septemba, aliandaa mkutano wa kwanza kabisa wa hali ya hewa barani Afrika katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, ambao ulimalizika kwa tamko la pamoja la kutaka mataifa yanayoongoza katika uchafuzi wa mazingira duniani kutoa rasilimali zaidi kusaidia mataifa maskini.
Licha ya hayo, aadhi ya wanamazingira wamemtaja rais Ruto kuwa mnafiki kwa kutetea upandaji miti huku akikosa kudhibiti ukataji miti ovyo katika misitu ya umma.
Mwezi uliopita, mahakama ya mazingira ilisitisha agizo ambalo Ruto la mwezi Juni kuondoa marufuku ya 2018 ya ukataji miti.