Pata taarifa kuu

Jeshi la Gabon latangaza uchaguzi kufanyika Agosti 2025

Wanajeshi waliompindua Rais Ali Bongo msimu huu wa kiangazi wametangaza kwamba uchaguzi wa urais na chaguzi zingine zitafanyika Agosti 2025, wakibainisha hata hivyo kwamba ratiba hii itawasilishwa kwenye mkutano wa kitaifa utakaojumuisha "wadau wote".

Rais wa mpito nchini Gabon, Brice Oligui Nguéma, sasa akivalia mavazi ya kiraia.
Rais wa mpito nchini Gabon, Brice Oligui Nguéma, sasa akivalia mavazi ya kiraia. © Communication présidentielle du Gabon
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wamapinduzi ya Agosti 30, Jenerali Brice Oligui Nguema, aliyetangazwa Rais wa Mpito na jeshi, aliahidi mara moja kurudisha mamlaka kwa raia baada ya kipindi cha mpito, lakini alikuwa bado hajafanya hivyo, na hakuweka muda.

Ni wachache walimkosoa kwa hili, kwani anapendwa na watu wengi wa Gabon kwa kukomesha miaka 55 ya "utawala wa Bongo" katika nchi iliyoathiriwa na ufisadi uliokithiri. Ikiwa ratiba iliyotangazwa Jumatatu itaheshimishwa, "kipindi cha mpito" kitadumu miaka miwili.

Katika hali ambayo tawala kadhaa za kifikra barani Afrika tayari zimeongeza muda wa kipindi cha mpito kuelekea kwenye uchaguzi, utawala wa kijeshi wa Libreville utachunguzwa kwa karibu na jumuiya ya kimataifa. Wao wamenufaika, ikilinganishwa na nchi zingine za Kiafrika huusan nchi za Afrika Magharibi amabzo zilitumia njia hiyo ya mapinduzi kushikilia madaraka.

"Mazungumzo ya pamoja"

"Agosti 2025: uchaguzi na mwisho wa kipindi cha mpito," msemaji wa mamlaka ya kijeshi, Luteni Kanali Ulrich Manfoumbi Manfoumbi, ametangaza moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali Jumatatu usiku, akiorodhesha "muda rasmi wa kipindi cha mpito (. ..) uliopitishwa na Baraza la Mawaziri". Lakini hii inabaki kuwa "dalili", kuwasilishwa kwa "mazungumzo ya kitaifa Jumuishi" mnamo mwezi wa Aprili 2024 ikijumuisha "wadau wote".

Usiku wa Agosti 30, alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais, Ali Bongo Ondimba alipinduliwa bila upinzani wowote au mapigano yoyote kati ya jeshi na takriban maafisa wakuu wote wa jeshi na polisi walikusanyika kumzunguka jenerali Brice Oligui Nguema, aliyetangaza Rais wa mpito siku mbili baadaye huku kukiwa na shangwe nderemo zikipigwa kote nchini.

Vyama vyote vya siasa, kikiwemo cha Bw. Bongo, pamoja na idadi kubwa ya mashirika ya kiraia, mara moja walijiunga na mamlaka ya Jenerali Nguema na kusifu sio "mapinduzi" bali "mapinduzi ya ukombozi", kulingana na neno walilotumia wafuasi jeshi lililofanya mapinduzi. Bwana Bongo alichaguliwa miaka 14 iliyopita, baada ya kifo cha babake Omar Bongo Ondimba mwaka 2009, ambaye alitawala nchi hii ndogo ya Afrika ya kati, yenye utajiri mkubwa wa mafuta, kwa zaidi ya miaka 41.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.