Pata taarifa kuu

Malema amshutumu rais Ruto kwa kwenda kinyume na ahadi alizotoa wakati wa kampeni

Nairobi – Mwanasiasa wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema amemkashifu rais wa Kenya William Ruto kwa kukosa kutimiza ahadi zake kwa raia wa taifa hilo la Afrika Mashariki wakati wa kampeni za kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

Julius Malema
Malema aidha katika hotuba yake, aliendelea kumshutumu rais Ruto kwa kutekeleza mambo tofauti na alivyoahidi. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza siku ya Alhamisi katika uzinduzi wa Taasisi ya Pan African nchini Kenya, Malema alimshutumu Rais Ruto kwa kuachana na malengo  yake ya kuongoza mchakato kuondoa suala ya matumizi ya dola ya Marekani kama chombo za biashara barani Afrika.

Pia alimsuta kiongozi huyo wa Kenya kwa kuunga mkono Israel katika mzozo wa Gaza
Pia alimsuta kiongozi huyo wa Kenya kwa kuunga mkono Israel katika mzozo wa Gaza REUTERS/Siphiwe Sibek

Malema aidha katika hotuba yake, aliendelea kumshutumu rais Ruto kwa kutekeleza mambo tofauti na alivyoahidi.

"Sijui kile ambacho rais William Ruto anamaanisha kwa sababu alisema mambo mengi na siwezi kumuelewa siku hizi kwa sababu mambo aliyosema wakati wa uchaguzi na anayofanya sasa ni mambo mawili tofauti," alisema Malema.

Utawala wa Ruto umekabiliwa na ukosoaji mkubwa kuhusu gharama ya maisha inayozidi kupanda licha ya kwamba rais alishinda uchaguzi mwaka jana kwa ahadi ya kupunguza na kukabiliana na athari za mfumuko wa bei za bidhaa.

Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha
Raia wa Kenya wamekuwa wakitoa kwa serikali ya Ruto kushugulikia suala la kupanda kwa gharama ya maisha REUTERS - MONICAH MWANGI

Rais, hata hivyo, ametetea sera zake za kiuchumi ambazo zinakashifiwa na baadhi ya wakenya, akisema alikuwa anapunguza deni la umma ambalo mtangulizi wake alikopa.

Malema, ambaye ni kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF), chama cha tatu kwa ukubwa katika bunge la kitaifa nchini Afrika Kusini, pia alimkashifu rais Ruto kwa kuwakaribisha kwa furaha Mfalme Charles III na Malkia Camilla wakati wa ziara yao ya hivi majuzi nchini Kenya.

Malema pia amemkashifu rais Ruto kwa kutomshinikiza mfalme wa Uingereza kuzungumzia dhuluma za wakati wa ukoloni
Malema pia amemkashifu rais Ruto kwa kutomshinikiza mfalme wa Uingereza kuzungumzia dhuluma za wakati wa ukoloni REUTERS - PHIL NOBLE

Mwanasiasa huyo wa upinzani nchini Afrika Kusini katika hotuba yake, alisema Mfalme wa Uingereza hakuelezea kujutia kwa ukatili uliofanywa wakati wa ukoloni wa Uingereza nchini Kenya.

Katika ziara hiyo, Mfalme Charles alielezea masikitiko yake kwa dhuluma zilizofanyika wakati wa ukoloni nchini Kenya lakini hakuomba msamaha rasmi.

Pia alimsuta kiongozi huyo wa Kenya kwa kuunga mkono Israel katika mzozo wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.