Pata taarifa kuu

DRC:Wanajeshi wawili wa Uganda wauwawa katika shambulio la wanamgambo wa ADF

Waasi wanaoungwa mkono na kundi la Islamic State wamewauwa wanajeshi wawili wa Uganda katika shambulio ambalo pia lilisababisha vifo vya raia wawili na mshukiwa wa shambulio mashariki mwa DR Congo.

Wanajeshi wa Uganda wafika karibu na mpaka na DRC kufuatia vita na waasi wa ADF mwezi Machi 2007.
Wanajeshi wa Uganda wafika karibu na mpaka na DRC kufuatia vita na waasi wa ADF mwezi Machi 2007. Photo: AFP Photo/Peter Busomoke
Matangazo ya kibiashara

Madereva wawili wa lori,Mkenya na Mkongo, wameuawa kwa kupigwa risasi Ijumaa usiku na kundi la Allied Democratic Forces (ADF) lenye washirika wa IS katika maegesho ya magari huko Kasindi, eneo la Beni.

Kasindi lilikuwa eneo la shambulio la bomu la kanisa la Pentekoste lililolaumiwa na ADF ambayo iliua takriban watu 15 Januari iliyopita, na ambayo kundi la  IS ilidai kuhusika nayo.

Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) zilianzisha opêresheni ya pamoja mwaka 2021 dhidi ya ADF ili kuwafukuza wanamgambo hao kutoka katika ngome zao za Kongo, lakini mashambulio bado  yanaendelea.

Hapo awali wakiwa na waasi wengi wa Kiislamu kutoka Uganda, ADF walipata umaarufu katika eneo hilo katika miaka ya 1990 na wanatuhumiwa kuwachinja maelfu ya raia.

Raia 26 walikufa usiku wa kuamkia Jumatatu-Jumanne katika mauaji yanayohusishwa na ADF karibu na mji wa Oicha, pia katika eneo la Beni, ambao umekuwa kitovu cha hujuma ya miaka mingi ya ADF, inayoitwa Jimbo la Kiislamu la Jimbo la Afrika ya Kati na IS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.