Pata taarifa kuu

Marekani yasitisha misaada ya kifedha kwa nchi ya Gabon

Marekani imetangaza kusitisha misaada mingi ya kifedha kwa nchi ya Gabon kufuatia mapinduzi ya kijeshi ya mwezi Agosti lakini imesema iko tayari kutoa msaada kwa ajili ya maendeleo madhubuti kuelekea demokrasia. 

Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye sasa ni rais wa muda wa Gabon, akiwapungia mkono magari ya kijeshi wakati wa gwaride la kijeshi, mjini Libreville, Septemba 4, 2023.
Jenerali Brice Oligui Nguema, ambaye sasa ni rais wa muda wa Gabon, akiwapungia mkono magari ya kijeshi wakati wa gwaride la kijeshi, mjini Libreville, Septemba 4, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Marekani ambayo tayari ilikuwa imesitisha usaidizi baada ya kutwaa mamlaka ya kijeshi, imesema imeamua rasmi kuwa mapinduzi yalifanyika, ambayo kwa mujibu wa sheria za Marekani yanataka kukomeshwa kwa misaada isiyo ya kibinadamu.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Matthew Miller amesema katika taarifa yake kwamba Marekani itaendelea wake pamoja na hatua madhubuti za serikali ya mpito kuelekea kuanzisha utawala wa kidemokrasia,""Marekani inasimama na watu wa Gabon katika matarajio yao ya demokrasia, ustawi na utulivu." amesisitiza

Tofauti na Niger, nchi nyingine ya Kiafrika ambako Marekani hivi karibuni ilikata misaada kwa sababu ya mapinduzi, msaada wa Marekani umekuwa mdogo kwa Gabon, ambayo ina utajiri mkubwa wa mafuta na iliendeshwa na familia ya Bongo kwa zaidi ya nusu karne.

Viongozi wa kijeshi wa Gabon walimpindua Ali Bongo Ondimba baada tu ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi ulioshutumiwa na watu wengi kwa makosa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.