Kenya: Mahakama yaongeza muda wa kusitisha kutumwa kwa Vikosi vya usalama Haiti
Mahakama kuu nchini Kenya, imeongeza muda wa kuzuia serikali kuwatuma polisi wake nchini Haiti kukabiliana na makundi ya magenge nchini humo.
Imechapishwa:
Ni uamuzi unaojiri wakati huu umoja wa mataifa ukisema usalama nchini Haiti umedorora zaidi, ambapo makundi ya magenge yanathibiti baadhi ya miji.
Nchi ya kenya ilikuwa imejitolea kuongoza ujumbe wa umoja wa mataifa kudhibiti magenge hayo nchini Haiti, ila mwanasiasa wa upinzani Ekuru Aukot, akafika mahakamani kupinga hatua hiyo kwa misngi kuwa katiba ya Kenya hairuhusu polisi wake 1000, kutumwa nje ya nchi.
Bunge lilistahili kuidhinisha kutumwa polisi hao nchini Haiti, mawakili wa bunge la Kenya wamesema bunge haliwezi kujadili swala ambao lipo mbele ya mahakama.
Kenya ilichukuwa hatua ya kutaka kuwatuma wanajeshi wake kule haiti kutokana na wito wa waziri mkuu Ariel Henry, kutraka jamii ya kimataifa kuisadia nchi yake.