Pata taarifa kuu

Gabon: Mke  Ali Bongo, Sylvia Bongo amefungwa jela

Mke wa rais aliyeondolewa madarakani nchini Gabon Ali Bongo Ondimba, amabye amekuwa chini ya kifungo cha nyumbani tangu mapinduzi ya kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika ya kati mwishoni mwa Agosti, amefungwa jela, wakili wake amethibitisha.

Mke wa Bongo alishtakiwa Septemba 28 kwa utakatishaji fedha na kughushi rekodi.
Mke wa Bongo alishtakiwa Septemba 28 kwa utakatishaji fedha na kughushi rekodi. AFP - GABRIEL BOUYS
Matangazo ya kibiashara

Sylvia Bongo Ondimba Valentin, anayeshukiwa kuhusika na ubadhirifu wa fedha za umma, alifungwa jela siku ya Jumatano, wakili wake Francois Zimeray amesema.

Mke wa Bongo alishtakiwa Septemba 28 kwa utakatishaji fedha na kughushi rekodi.

Sylvia Bongo amekuwa amekuwa akizuiliwa nyumbani katika mji mkuu, Libreville, tangu mapinduzi ya Agosti 30 yalionagusha utawala miaka 55 wa familia ya Bongo.

Aidha wawili hao wanatuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa za umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita
Aidha wawili hao wanatuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa za umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita © AFP/Steeve Jordan

Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa zamani wa nchi na wapambe wake walighushi matokeo ya uchaguzi.

Wanamshutumu Sylvia Bongo na mwanawe, Nourredin Bongo Valentin, kwa kumdanganya rais huyo wa zamani, ambaye hajapona kabisa kutokana na kiharusi kikubwa alichokabiliwa nacho mwaka wa 2018.

Aidha wawili hao wanatuhumiwa kwa kutumia vibaya pesa za umma katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa zamani wa nchi na wapambe wake walighushi matokeo ya uchaguzi
Inadaiwa kuwa kiongozi huyo wa zamani wa nchi na wapambe wake walighushi matokeo ya uchaguzi © STEEVE JORDAN / AFP

Bongo, 64, ambaye alikuwa ameongoza taifa hilo la Afrika ya kati tangu mwaka wa 2009, aliondolewa madarakani na wanajeshi saa chache baada ya kutangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa urais.

Ali Bongo alichaguliwa baada ya baba yake kufariki mwaka wa 2009 baada ya kuongoza kwa karibia miaka 42.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.