Pata taarifa kuu

Majadiliano kuhusu ufadhili wa tume ya walinda amani wa AU yameanza

Nairobi – Baraza la usalama la umoja wa Mataifa na lile la umoja wa Afrika, hapo jana walianza majadiliano kuhusu ufadhili wa tume za kulinda amani zilizoko chini AU barani Afrika.

Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na operesheni za aina gani zitafadhiliwa
Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa ni pamoja na operesheni za aina gani zitafadhiliwa AFP - AMANUEL SILESHI
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Afrika, unaoundwa na nchi wanachama 55 na idadi ya watu wanaofikia bilioni 1 na laki 4, kwa muda sasa imekuwa ikikabiliwa na tatizo la ufadhili wa operesheni zake za kulinda amani, kutokana na kuzitegemea nchi washirika kama umoja wa Ulaya.

Kamishena wa AU anayehusika na masuala ya kisiasa, amani na usalama, Bankole Adeoye, amesema imefika wakati taasisi hiyo kuwa na mikakati endelevu ya kifedha, ili kukabili shida za usalama zinazosumbua bara hilo kwa sasa.

Kwa muda sasa ajenda hii imekuwa mezani mwa baraza la usalama la umoja wa Mataifa, ambapo nchi za Afrika zinataka kuwe na kipengele cha kuzilazimisha nchi wanachama kuchangia operesheni zake.

Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa katika ajenda hii iliyoanza tangu mwaka 2018, ni pamoja na operesheni za aina gani zitafadhiliwa, pamoja na namna ya kuwawajibisha wahusika watakaobainika kutumia fedha hizo vibaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.