Pata taarifa kuu

Gabon: Kiongozi wa mapinduzi amekutana na rais wa Kongo-Brazzaville

Kiongozi wa mapinduzi ya kijeshi Gabon amefanya mazungumzo na rais wa Kongo Denis Sassou Nguesso wakati huu akijaribu kutafuta namna ya kuondoa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya nchi hiyo na kutengwa kimataifa.

Kiongozi wa kijeshi wa Kongo anajaribu  kutafuta namna ya kuondoa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya nchi hiyo na kutengwa kimataifa
Kiongozi wa kijeshi wa Kongo anajaribu kutafuta namna ya kuondoa vikwazo vilivyotangazwa dhidi ya nchi hiyo na kutengwa kimataifa © Loïcia Martial/RFI
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Brice Oligui Nguema alisema ziara yake ya Jumapili nchini Kongo-Brazzaville ililenga kuimarisha uhusiano na majirani zake na kuondoa kutengwa kwa Gabon ndani ya eneo hilo na kimataifa.

Hatua hii inakuja wiki kadhaa baada ya uanachama wa Gabon katika Umoja wa Afrika  na muungano wa mataifa ya Afrika ya Kati, ECCAS, kusimamishwa baada ya mapinduzi ya Agosti 30.

ECCAS pia ilihamisha makao yake makuu kutoka Gabon hadi Equatorial Guinea baada ya mapinduzi.

Jenerali Oligui alisema alikuwa amefanya mashuriano na  rais Nguesso, majadiliano aliyoyataja kama ya manufaa kwa nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.