Pata taarifa kuu

Somalia: Raia watano wameuawa kwenye shambulio la kigaidi

Raia watano wameripotiwa kuawaua wakati wengine kumi na watatu wakijeruhiwa katika mlipuko wa gari katikati mwa nchi ya Somalia.

Wapiganaji wa al-Shabab kwa mara kadhaa wamekuwa wakiwalenga raia na maofisa wa jeshi kwenye taifa hilo
Wapiganaji wa al-Shabab kwa mara kadhaa wamekuwa wakiwalenga raia na maofisa wa jeshi kwenye taifa hilo REUTERS/Feisal Omar/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa maofisa wa polisi, gari ambalo lilikuwa na vilipuzi, lililipuka karibu na soko lenye shughuli nyingi katika wilaya ya Buloburde eneo la  Hiran.

Wapiganaji wa al-Shabab kwa mara kadhaa wamekuwa wakiwalenga raia na maofisa wa jeshi kwenye taifa hilo linalokabiliwa na utovu wa usalama kutoka kwa kundi hilo na washirika wake.

Rais wa Somali Hassan Sheikh Mohamud, hivi karibuni, alianzisha awamu ya pili ya vita dhidi ya kundi hilo la al-Shabab ambalo limesababisha mauaji ya raia katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Al-Shabab wameokana kuwa tishio kwa usalama wa mataifa jirani na Somali, Kenya ikiwa mojawapo ya mataifa yalioathirika pakubwa na mashambulio hayo, kaunti jirani na Somali upande wa Kenya zikishambuliwa mara kwa mara.

Serikali ya Mogadishu kwa msaada wa wanajeshi wa Umoja wa Afrika na mifumo ya anga ya Marekani, imechukua maeneo kadhaa yaliokuwa yanakaliwa na wapiganaji hao.

Licha ya kuchukua maeneo hayo, wapiganaji hao wameripotiwa kuimarisha vita dhidi ya wanajeshi wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.