Pata taarifa kuu

Ombi la Somalia kuhusu vikosi vya ATMIS laungwa mkono na nchi wanachama

Nairobi – Nchi zinazochangia vikosi vya ujumbe wa Afrika wa kulinda amani nchini Somali, ATMIS, zimeunga mkono ombi la nchi hiyo la kutaka mpango wa kuwaondoa wanajeshi wa kikosi hicho nchini humo kucheleweshwa kwa miezi mitatu kutokana na hofu ya kulegea kwa vita dhidi ya magaidi.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa wanajeshi elfu 3 waliokuwa waondoke nchini Somalia kufikia hivi leo, wataendelea kusalia nchini humo
Hatua hiyo inamaanisha kuwa wanajeshi elfu 3 waliokuwa waondoke nchini Somalia kufikia hivi leo, wataendelea kusalia nchini humo AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Hatua ya Kenya, Ethiopia, Djibouti, Uganda na Burundi sasa inamaanisha kuwa wanajeshi elfu 3 waliokuwa waondoke nchini Somalia kufikia hivi leo, wataendelea kusalia nchini humo, au wabadilishwe na idadi ya wanajeshi sawa na hiyo, ili kuziba mianya ya kiusalama katika maeneo ambayo vikosi hivyo vitaondoka.

Nchi hizo zimeiambia baraza la usalama la umoja wa mataifa kwamba wanaunga mkono kusitishwa kwa hatua ya kuondoka kwa wanajeshi kwa sababu wanakubalian ana Mogadishu kuwa taifa hilo linahitaji muda kushughulikia mappungufu ya kiusalama iliopo, ikiwemo idadi ya wanajeshi wa kutoka kutekeleza majukumu ya kiusalama.

Hata hivyo, nchi hizo zimasema kuwa suala la ufadhili ni la dharurua na ni sharti liangaziwe ili kuhakikisha vikosi vyao vinaendelea kusalia nchini Somalia. 

Baraza la usala la UN linatarajiwa kuhjadili suala hilo, hata hivyo baraza la amani na usalama lla Umoja wa Afrika linatakiwa kuongoza majadiliano ya namna ya kuendelea kufadhili vikosi hivyo baada ya hivi leo tarehe 29 Septemba. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.