Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Gabon: Mke wa rais aliypinduliwa Ali Bongo ashtakiwa kwa 'utakatishaji wa fedha haramu'

Karibu mwezi mmoja baada ya mapinduzi ambayo yaling'oa mamlakani rais wa zamani Ali Bongo, mkewe, Sylvia Bongo, ameshtakiwa kwa 'utakatishaji wa fedha haramu, wizi na kughushi nyaraka mbalimbali'.

Mke wa rais wa zamani wa Gabon, Sylvia Bongo Ondimba, akihudhuria mechi ya kandanda ya Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 kati ya Gabon na Guinea-Bissau kwenye Uwanja wa Urafiki wa China na Gabon kutoka Libreville Januari 14, 2017.
Mke wa rais wa zamani wa Gabon, Sylvia Bongo Ondimba, akihudhuria mechi ya kandanda ya Kundi A Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 kati ya Gabon na Guinea-Bissau kwenye Uwanja wa Urafiki wa China na Gabon kutoka Libreville Januari 14, 2017. AFP - GABRIEL BOUYS
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mwendesha mashtaka André Patrick Roponat, Sylvia Bongo alisikilizwa mnamo Septemba 28, 2023 na jaji anayechunguza tuhuma zinazomkabili. Hapa sasa anashtakiwa kwa "utakatisha wa fedha haramu, wizi, na kughushi nyaraka mbalimbali". Amewekwa nchini ya kifungo cha nyumbani.

Hali yake imefafanuliwa, tangu mapinduzi ya Agosti 30, Sylvia Bongo, mwenye uraia pacha (Gabon na Ufaransa) anawekwa mahali pasipojulikana, bila kujua hatima yake. Mawakili wake pia waliwamewasilisha malalamiko nchini Ufaransa kwa mteja wao kuwekwa kizuizini kiholela na wanalaanikuendelea kushikwa mateka.

Waangalizi wengi wanashuku Sylvia Bongo kuwa katikati mwa mfumo mkubwa wa ufisadi kwenye ngazi ya juu serikalini.

Mara tu baada ya mapinduzi, msaidizi wake Kim Oun alikamatwa nyumbani kwake. mabegi yaliyojazwa pesa yalikamatwa ofisini kwake na szehemu zingine. Mtu huyo alisema kuwa fedha hizo ni za Sylvia Bongo, na kwamba ofisi hiyo ilikuwa ikisimamiwa na yeye  moja kwa moja.

Kwa hali yoyote, mashtaka haya humenyuka. Geoffroy Foumboula ni msemaji wa kundi la mashirika yasiyo ya kiserikali, ambaye alitangaza mfululizo wa malalamiko dhidi ya mke huyo wa rais aliyetimuliwa mamlakani Ali Bongo. Anazungumza juu ya "habari njema" na "ishara kali". Sasa anatarajia kwamba "maagizo yataenda vizuri hadi mwisho". Kulingana na Geoffroy Foumboula, mahakama itaendelea na shughuli zake, hadi kwa Ali Bongo mwenyewe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.