Pata taarifa kuu

Gabon: Marekani yasitisha misaada yake kwa Gabon

Nairobi – Marekani imesema kwamba itasitisha misaada yake kwa nchi ya Gabon baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi uliopita nchini humo.

Marekani imesema kwamba itasitisha misaada yake kwa nchi ya Gabon baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi uliopita nchini humo
Marekani imesema kwamba itasitisha misaada yake kwa nchi ya Gabon baada ya jeshi kuchukua madaraka mwezi uliopita nchini humo © RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken jumanne ya wiki hii alisema serikali yake imesitisha baadhi ya programu za usaidizi zinazonufaisha serikali ya Libreville huku ikitathmini uingiliaji kati usio wa kikatiba wa wanajeshi wa nchi hiyo.

Hata hivyo, Blinken amesema kuwa Marekani inadumisha operesheni za kidiplomasia na kibalozi katika nchi hiyo yenye utajiri wa mafuta ya Afrika ya Kati, na kwamba hatua ya kusitisha misaada kwa sasa ni ya muda.

Awali maafisa wa Marekani walisema kwamba msaada wa Marekani ulikuwa mdogo kwa serikali ya Gabon, inayoendeshwa na familia ya Bongo kwa zaidi ya nusu karne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.