Pata taarifa kuu

Burna Boy ameahirisha tamasha lake lililopangwa kufanyika Afrika Kusini

Msanii wa Nigeria Burna Boy ameahirisha tamasha la moja kwa moja lililopangwa kufanyika wikendi hii jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Tamasha hilo sasa litafanyika mwezi Desemba
Tamasha hilo sasa litafanyika mwezi Desemba © DR Atlantic Records
Matangazo ya kibiashara

Onyesho hilo, ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika katika uwanja wa FNB wenye uwezo wa kutoa nafasi kwa watu 90,000 sasa litafanyika Desemba 16, kwa mujibu wa wakala wa tikiti wa hafla hiyo.

Kwa mujibu wa Ticket Pro, tamasha hilo limesongezwa mbele kwa sababu ya kukosekana kuuzwa kwa tikiti miongoni mwa sababu zingine.

Kwa upande wake, kampuni ya usimamizi ya Burna Boy, Spaceship, imenukuliwa na vyombo vya habari vya Nigeria ikilaumu wapangaji  wa tamasha hilo kwa kutotimiza kile ambacho imesema ni majukumu yao ya kimkataba, kifedha, uzalishaji na kiufundi".

Taarifa hiyo inataka kampuni za tikiti zihakikishe kuwa waliokuwa wamenunua  tikiti wanarejeshwa kikamilifu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.