Pata taarifa kuu

Afrika yaaboresha mahitaji yake ya hali ya hewa: ufadhili, madeni na kodi

Mkutano wa kwanza wa kilele wa tabianchi barani Afrika uliandaa wiki hii mjini Nairobi orodha ya mahitaji ya Afrika kupunguza mzigo wa kifedha wa mapambano dhidi ya ongezeko la joto duniani. Kufadhili nishati mbadala, mageuzi ya mfumo wa fedha wa kimataifa na kodi ya kaboni, hayo ni baadhi ya mahitaji yaliyopendekwezwa katika mkutano huo.

Rais wa Kenya William Ruto akihutubia wajumbe wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kilele wa tabianchi barani Afrika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta jijini Nairobi, Septemba 6, 2023.
Rais wa Kenya William Ruto akihutubia wajumbe wakati wa kuhitimisha Mkutano wa Kilele wa tabianchi barani Afrika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Kenyatta jijini Nairobi, Septemba 6, 2023. © AP
Matangazo ya kibiashara

Katika "Azimio la Nairobi", bara la Afrika ambalo linachangia 2% hadi 3% tu ya uzalishaji wa gesi chafu duniani, limejitahidi kupata msimamo wa pamoja katika mchakato wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi, ambao utahitimishwa na mkutano wa tabianchi wa Umoja wa Mataifa (COP28) huko Dubai mwishoni mwa mwezi Novemba.

Pointi muhimu zilizopendekezwa:

Nishati safi

Mbali na uwezo wa asili wa kuzalisha moja kwa moja nishati safi (jua, upepo, jotoardhi, n.k.), Afrika ina 40% ya hifadhi ya dunia ya cobalt, manganese na platinamu, muhimu kwa betri na seli za mafuta ya hidrojeni.

Bara hili linanufaika tu na 2% ya uwekezaji wa mpito wa nishati duniani katika muongo mmoja uliopita.

Mkutano wa Nairobi ulitoa wito wa uwekezaji wa dola bilioni 600 ili kuongeza uwezo wa uzalishaji wa nishati mbadala barani Afrika kutoka gigawati 56 mwaka 2022 hadi angalau gigawati 300 ifikapo 2030.

Ni sharti kwa bara lenye wakazi bilioni 1.4, milioni 600 ambao hawana umeme.

Ushuru wa kaboni

Ili kusaidia kupata fedha zinazohitajika kwa uwekezaji huu, Azimio la Nairobi linatoa wito kwa viongozi wa dunia "kusimama nyuma ya pendekezo la mfumo wa ushuru wa kaboni ikiwa ni pamoja na ushuru wa biashara ya mafuta na usafirishaji wa baharini na anga".

Vyanzo hivi vya ufadhili, linaongeza Azimio, vinaweza kuongezwa na ushuru wa kimataifa wa miamala ya kifedha.

Wakati wa mkutano wa kilele mjini Paris mwezi Juni, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alizungumza na kuunga mkono kodi ya biashara ya baharini huku akisisitiza uanachama unaohitajika wa China, Marekani na nchi nyingine za Ulaya ili iwe imara.

Jijini Nairobi, mjumbe wa Marekani kuhusu tabianchi John Kerry alijiwekea kikomo kwa kueleza kwamba mapendekezo haya tofauti yalikuwa yanachunguzwa huko Washington.

Marekebisho ya mfumo wa fedha

Washiriki katika Mkutano wa Nairobi waliongeza sauti zao kwa wito wa kurekebisha usanifu wa mfumo wa fedha wa kimataifa, ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliuelezea kuwa "uliopitwa na wakati, usio wa haki na usiofanya kazi."

Viongozi hao pia walitoa wito wa marekebisho na msamaha wa madeni kwa nchi zao. Mzigo wa madeni barani Afrika umeongezeka kutokana na janga la Uviko-19, uvamizi wa Urusi nchini Ukraine na athari za tabianchi, kulingana na Tume ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika.

Hata hivyo, upatikanaji wa fedha kutoka IMF na Benki ya Dunia unachukuliwa kuwa mgumu na nchi zinazoendelea, zinakabiliwa na changamoto ya kuondoa sehemu kubwa ya wakazi wao kutoka kwenye umaskini huku zikijikomboa kutoka kwa nishati ya mafuta.

Marekebisho ya taasisi hizo mbili yanapaswa kuwa kiini cha mkutano wao wa kila mwaka mnamo mwezi Oktoba huko Marrakech.

Uchumi usio na kaboni

Nchi za Kiafrika zimetaka ukuaji wa uchumi utegemee kidogo nishati ya mafuta, zaidi ya mtindo wa "kijadi" wa maendeleo ya viwanda.

Kiini cha mkakati huu: kuhakikisha kwamba malighafi ya bara hili inajaa kwa wingi, ikiwa ni pamoja na madini yanayotumika kwa teknolojia ya kijani kibichi, yanabadilishwa ndani na si kusafirishwa tu.

Chaguo jingine litakuwa kuchuma mapato vyema kwa mifumo mikubwa ya ikolojia ya bara - misitu, mikoko, ardhi oevu - ambayo inachukua CO2 kwenye soko la mikopo ya kaboni.

Lakini soko hili, ambalo limedhibitiwa vibaya, ndilo linalolalamikiwa, huku baadhi ya miradi - hasa misitu - ikiwa na, kulingana na wapinzani, athari ndogo katika kuhifadhi mazingira au ulinzi wa jamii za mitaa.

"Mikopo ya kaboni ni 'ruhusa ya kuchafua'," amesema Mohamed Adow, mkurugenzi wa shirika la Power Shift Africa.

Athari za hali ya hewa

Mataifa ya Afrika yamezikumbusha nchi tajiri zinazochafua mazingira kuheshimu ahadi yao, iliyotolewa mwaka 2009, ya kutoa dola bilioni 100 kwa mwaka katika ufadhili wa tabianchi ifikapo mwaka 2020.

Pamoja na kusaidia nchi zilizo hatarini zaidi kukabiliana na athari za mara moja za mabadiliko ya tabianchi kupitia hazina iliyopitishwa katika COP27 nchini Misri, inayolenga mataifa tajiri kufidia "hasara na uharibifu" wa mataifa Kusini.

Kauli moja

Wakuu wa nchi za Nigeria na Afrika Kusini, watu wawili wenye nguvu katika bara hilo ambao uchumi wao unategemea nishati ya mafuta, hawakuhudhuria mkutano huo.

Lakini Umoja wa Afrika umehakikisha kuwa Azimio la Nairobi lilipitishwa kwa kauli moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.